Burundi hali si shwari tuwaombee hao ndugu zetu wa Magharibi

Burundi hali si shwari tuwaombee hao ndugu zetu wa Magharibi

The Supreme Conqueror

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2017
Posts
458
Reaction score
1,280
Wakuu habari za muda huu nimeona nifungue uzi huu kwa lengo la kujadili kwa mapana haya yanayoendelea nchi ni Burundi baada ya Ijumaa ya wiki jana Rais wa nchi hiyo kutamka hadharani kuwa kuna baadhi wa viongozi wa juu wa serikali yake kutamani kiti chake cha urais na jana Rais Everiste kutangaza kumfuta kazi Waziri Mkuu wake ikiwa ni muendelezo ya yale aliyotaka Ijumaa.

je, Hao ndugu zetu wataingia katika machafuko mengine na jaribio la mapinduzi ya Rais akiwa madarakani kwa mara ya 3 ikiwa ni 2 huko nyuma ikihusisha mauaji ya Marais 2 wakiwa madarakani?

Karibuni tuchangie wadau.
 
Wakitifuana Balaa ni mikoa ya Magharibi Huko ujambazi Utarudi kuwa mkubwa zaidi
 
Hakuna vita tena huko mi naona km kwa mbali wanaanza kukomaa kisiasa naona leo p.m mpya ameapishwa
 
Na sisi waafrika upumbavu na ujinga umezidi kipimo.
Uchu wa madaraka umekuwa ulevi wa wanasiasa..

Ifikie hatua tuwaache wauane pengine itafikia hatua waseme inatosha japo watakao kufa sio vuongozi Ni wananchi.
Hii sio kauli nzuri ya kuombea watu walio hai. kumbuka mtu mmoja au kikundi tuu cha watu kati ya watu milion hamsini wanaweza leta machafuko. sasa tuingiliapo na kuleta amani ndipo tunawakomoa hao wachache wenye kutaka kudhulumu haki za wengine, wewe huoni Israel haiui watu wasio na hatia bali wale wachache tuu wasio amini suluhisho la amani. yupo wapi Moahamedi mahbor, Mohamedi hamshari, Nawatif hawatmeh, Abdelman Ranzizi, sheikh yasin na Abu Jihad?
 
Nyani waliochangamka Kwny shamba la bwana heri 😄😄
 
Hii sio kauli nzuri ya kuombea watu walio hai. kumbuka mtu mmoja au kikundi tuu cha watu kati ya watu milion hamsini wanaweza leta machafuko. sasa tuingiliapo na kuleta amani ndipo tunawakomoa hao wachache wenye kutaka kudhulumu haki za wengine, wewe huoni Israel haiui watu wasio na hatia bali wale wachache tuu wasio amini suluhisho la amani. yupo wapi Moahamedi mahbor, Mohamedi hamshari, Nawatif hawatmeh, Abdelman Ranzizi, sheikh yasin na Abu Jihad?
Kwamba israel? Huyo Israel keani nani anampa hiyo haki ya kukalia ardhi za wengine na hata kujichagulia yeye kwa raha zake wasiotaka suluhisho la amani na kuwauwa?

Wewe hujui kuwa wapigania uhuru wote wakiwamo kina Mandela, Mugabe, Kenyatta na wengine wote kwa mabeberu walikuwa ni wasio taka suluhisho la amani?

Kwa taarifa yako uliowaorodhesha hapo kwa wapigania uhuru, wote ni mashujaa.

RIP Mohammed Hamshari na wenzako.
 
Shida nini kwa hawa majirani zetu? Kwanini wanapinduana sana?
 
Back
Top Bottom