Burundi: Pierre Nkurunziza kuzikwa leo

Burundi: Pierre Nkurunziza kuzikwa leo

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Mwili wa aliyekuwa Rais wa Burundi hayati Pierre Nkurunziza unazikwa leo kwenye makaburi ya mji wa Gitega ,mji mkuu wa kisiasa ulioko katikati mwa Burundi

Hafla ya mazishi zinatarajiwa kuongozwa na Rais mpya Jenerali Evariste Ndayishimiye na wakuu wengine wa serikali.

Hayati Nkurunziza alifariki dunia tarehe 8 mwezi huu ,miezi miwili kabla ya kukabidhi madaraka kwa mrithi wake kufwatia uchaguzi uliofanyika mwezi wa tano.

Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa na serikali ya Burundi, hafla itaanzia kwenye 'hospital du Cenquantenaire Twese Turashoboye' iliyoko kwenye mkoa wa Karusi ambako maiti yake imehifadhiwa.

Mlolongo wa magari yatakayosindikiza maiti yake utatoka kwenye hospitali hiyo utatoka Karusi na kuelekea katika mji wa Gitega ambao ni mji mkuu wa kisiasa katikati mwa Burundi.

Wananchi wameomba kusimama kwenye barabara kumuaga marehemu.

Kunatarajiwa hafla fupi ya jeshi kumtolea heshma za mwisho kwenye uwanja wa mpira wa Ingoma mjini Gitega,kabla ya mwili wake kupitishwa mbele ya wananchi watakaokuwa uwanjani humo kumwaga na baadae kufanyika maziko rasmi.

Tangazo la serikali ya Burundi linasema kwamba shughuli nyingine kama kuweka mashada ya maua kwenye kaburi lake au hotuba zitakazotolewa zitafahamishwa leo.

Rais Pierre Nkurunziza alifariki dunia tarehe 8 mwezi huu kutokana na mshtuko wa moyo kama ilivyotangazwa na serikali ya nchi hiyo.

1593144294797.png
 
Kwa hiyo wazee wetu waliokwenda kuhudhuria maziko wapo huko toka siku hiyo?
 
Kuuana na matatizo ya moyo yanawamaliza viongozi wengi Afrika
 
Back
Top Bottom