Burundi: Taifa dogo linaloendelea kuteswa na Vita

Burundi: Taifa dogo linaloendelea kuteswa na Vita

Comred Mbwana Allyamtu

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2016
Posts
351
Reaction score
887
BURUNDI NA KILE KILICHOITWA MAPINDUZI YA VIPINDI VYOTE, NDANI YAKE TUNAPATA MUSTAKABALI MZIMA WA PIERRE NKURUZINZA.

Na Comred Mbwana Allyamtu
Tuesday -25/9/2018

Jana niliona uchambuzi murua kabisa juu ya hali ya kisiasa nchini Burundi kwenye ukurasa wa rafiki yangu Mossi H. Bigirimana jambo lilonipelekea kuandika makala hii juu ya kile kilichoitwa mapinduzi ya kijeshi nchini Burundi. Binafsi naifahamu nchi ya Burundi vizuri sana, kwanza Nimewahi kuitembelea nchi hiyo zaidi ya mara tano (5) nakumbuka mara ya mwisho kuitembelea Burundi ilikuwa mwaka 2014.

Mwaka huo nilikaa Burundi kwa muda mrefu kidogo kipindi hicho nikiwa nafundisha shule (chuo) ya elimu ya watu wazima kilichopo jijini Bujumbura katika tarafa ya Buyenzi, nikipindi hicho nilipo fahamiana na watu kadhaa akiwemo Mossi Bigirimana nazani yeye anaweza kuthibitisha hili humu facebook. Kwa wakati wote huo Burundi ilikuwa nyumbani kwani nilikuwa mwenyeji katika maeneo kadhaa mjini humo ikiwa ni pamoja na maeneo ya Buyenzi (eneo la makazi ya watu wenye kuzungumza kiswahili), Bwiza (eneo la makazi ya wakongomani), Kamenge, Kanyosha, Nyakabiga, Mtakura, kinama na maeneo mengine mengi ya mji huo mkuu wa Bujumbura nchini Burundi naimani Mjukuu Wa Justina Mwafrika au Leonard Chakupewa Twin Chaks Jr. anaelewa nitajapo mitaa hiyo.

Miezi mitano baadae nilienda mikoani (njee ya jiji la Bujumbura) hasa mikoa ya Bururi (mji wa Rumonge), Makamba, Kitega, Chibitoke, Muyinga na Ngozi katika shughuri mbali mbali za kijamii nchini humo. Pamoja na kuzuru maeneo mengi eneo lilonivutia na kunifanya leo kuandika makala hii ni pale nilipokuwa Burundi nilitembelea makazi ya raisi Ndadaye lilopo eneo la mjini (Muville) mahali ambapo aliuwawa na maasi ya askari wa nchi hiyo katika mapinduzi yaliyotokea mwaka 1993, kupitia ziara yangu Ile kipindi hicho eneo hilo na andiko nilisoma hapo jana juu ya msururu wa mapinduzi nchini humo ndipo nimevutika kuandika makala hii leo.

Ukweli ni kwamba nchi ya Burundi ni moja ya nchi za kiafrika ambazo zimeshuhudia mapinduzi kadhaa toka uhuru wake mwaka 1962, Mbali na hilo lakin pia taifa hilo limekuwa likikumbwa na machafuko ya mara kwa mara ikiwemo yale ya mwaka 1961, 1963, 1966, 1968, 1972, 1993, 1994, 1997 na haya ya karibuni ya mwaka 2015.

Kihistoria Burundi ambayo huko nyuma ilijulikana kama Urundi ni eneo linalopatikana katika Afrika mashariki katika ukanda wa mashariki ya Afrika ya kati na imepakana na DRC kwa upande wa magharibi, kusini imepakana na ziwa Tanganyika na upande wa kaskazini imepakana na Rwanda huku upande wa mashariki imepakana na Tanzania hasa katika wilaya za Ngara kwa mkoa wa Kagera na kibondo iliyopo mkoa wa Kigoma.

Mji wake mkuu ni Bujumbura ambayo huko nyuma ulijulikana kama Usumbura wenyeji wa nchi hiyo ni kabila la Watwa (Batwa) ambao waliishi hapo toka miaka ya 300 BC na baadae kati ya miaka 110 AD na 340 AD walikuja jamii nyingine ya wabantu waliotoka kwenye misitu ya Kongo na Kameroni waliojulikana kama Wahutu (Hutu) ambao walitawanyika katika ukanda wote wa milima ya "Urundi" na walikuwa wawindaji na baadae wahamiaji wa kuhutu wakaanza kujihusisha na shuguri za kilimo mnamo miaka ya 600 AD.

Katikati ya miaka ya 900 AD jamii kubwa ya Nilotic kutoka kwenye kikundi cha jamii ya wafugaji ya Wahamatic iliyojulikana kama Watutsi (Tusi) ilianza kuvamia ukanda wote wa nyanda za mashariki ya Afrika ya kati, hatimaye mwaka 987 AD watutis walifika Burundi na kutapakaa maeneo yote ya nyanda za juu za ukanda unaojulikana kama Muranvya ambapo Waliweka makazi yao. Watusi walikuwa ni wafugaji wenye makundi makubwa ya ng'ombe ambao walikuwa nakitafuta makazi bora ya malisho kwa ajili ya mifugo yao.

Kuanza kwa uvamizi wa wazungu mwanzoni mwa miaka ya 1800 kuliifanya Burundi kutawaliwa na Ujerumani ambapo Burundi, Rwanda na Tanganyika zote zilikuwa ni nchi moja iliojulikana kama Ujerumani ya Africa mashaliki (German East Africa) ambapo baadae Burundi na Rwanda alipewa uberigiji mara baada ya vita ya kwanza ya dunia kumalizika ndipo Urundi yani Burundi na Urwanda yani Rwanda ndipo zilipo pewa koloni lingine la Uberigiji kwa kile kilichoitwa "Fidia ya kushindwa vita kwa Ujerumani" kupitia mkataba wa Anglo-Belgium Treaty 1919.

Ujio wa mbelgiji ndio chanzo cha kuibuka kwa matabaka baina ya makabila mkubwa mawili yani Wahutu na Watusi, hapa mbeligi alianza kuwatumia Watusi katika shuguli zake za kiutawala kama makalani, walimu,maafisa wa ngazi za chini na kuwapa fursa za kijamii tofauti na ilivyo kwa kabila la Wahutu waliowengi na hii ni kutokana na kabila la Wahutu walikuwa watu wakolofi, wabishi na wakali huku Watusi walikuwa watu wakimya, wapole na wastaalabu kitu kikichopelekea wazungu kuwapenda na kuwatumia katika shuguli za utawala jambo lililopelekea kuongezeka kwa chuki baina ya hayo makabila mawili yani Watusi na Wahutu kwani Watusi waliwanyanyapaa Wahutu kwa kiasi kikubwa na chuki hiyo iliongezewa chuki maradufu na wakoloni wa kizungu (Wabeligiji) kwakuwa karibu sehemu nyingi za utawala walipewa Watusi kama Askali wa usalama, Askali wa mageleza maafisa suluhu na sehemu nyigi za utawala.

Na ilipofika miaka ya 1949 wabeligiji waliona wa badiri mfumo wa utawala na kuanzisha mfumo mpya ulioitwa "Tribe classical system of administration" na hii ndio iliyo kuja kuchochea ukabila tunaouona ukiishi leo Burundi na Rwanda kwakuwa haya mataifa yanafanani kwa karibu kila kitu.

Kwa Burundi uberigiji aliwapa mamlaka Watusi na kuwabagua Wahutu huku kwa Rwanda katika miaka ya 1950 mbeligiji alianza kuwapa kipaumbele Wahutu kutokana na msukumo wa wamissionari wa kikatoriki walioanza kuwatetea Wahutu kwa kuona wao ndio wanaonyanyaswa na kubaguriwa hivyo uberigiji aliona ni vyema kuwapa msukumo Wahutu kwakuwa kipindi hicho vuguvugu la Wahutu lilikuwa kubwa.

Ubeligiji ndipo miaka ya 1950 kulianza kuzuka vuguvugu la ukombozi barani Afrika hata hivyo Burundi nayo aikubaki nyuma. Mwaka 1956 ndipo mtoto wa mfalme Mwabusta V (Mwami Mwambusa) aliojulikana kama mwana mfalme Prince Lous Rwagasore alipo unda chama cha ukombozi kilicho julikana kwa jina la UPRONA.

Mwaka moja kabla ya uhuru kulikuwa na uchaguzi wa kwanza chini ya usimamizi wa UN na chama mshindi kilikuwa ni UPRONA kilichoongozwa na mwanamfalme Mtutsi Louis Rwagasore aliyemwoa mwanamke wa Kihutu na chama kiliunganisha pande zote mbili za makabila hasimu ya wahutu na watutis, Lakini miezi michache baadaye Rwagasore aliuawa na chama chake kilitengana kufuatana na migogoro ya ukabila.

Baada ya mauaji ya Rwagasore mapema mwaka 1962 hatimae mzuka wa mapinduzi ulianza nchini humo Kwani Julai 1966, Mfalme Mwambutsa wa IV alipinduliwa na mwanawe akafanywa kuwa mfalme aliyeitwa Ntare wa V.

Naye Mfalme Ntare mwaka huo huo alipinduliwa katika mapinduzi ya kijeshi ya Novemba 1966 yaliyo ongozwa na Michel Micombero, ambaye alikuwa amechaguliwa Waziri Mkuu mwaka 1966 katika kile kilichokuwa kikitazamwa kama kupoza hali ya mambo baada ya machafuko kuzuka, baada ya mapinduzi Michombero akawa rais na Burundi kuwa jamuhuri huku Katiba mpya ikaanzishwa mwaka 1970.

Micombero naye alipinduliwa na Kanali Jean-Baptiste Bagaza mwaka 1976. Kisha Bagaza naye akapinduliwa na Pierre Buyoya mwaka 1987.Bagaza alitawala na yeye kuondolewa Kwenye mapinduzi ya tarehe 3 Septemba 1987 Jean-Baptiste Bagaza aliondolewa na Buyoya na nchi kuongozwa na kikundi cha kijeshi toka tarehe 3 Septemba 1987 mpaka tarehe 10 Julai 1993 chini ya Pierre Buyoya. Buyoya alitawala nchi mpaka katika mwanzo mpya wa kisiasa katika kuibuka kwa demokasia mwanzoni mwa miaka ya 1992 Kufatia hali hiyo uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia ukafanyika mwaka 1993.

Katika uchaguzi huu Melchior Ndadaye alishinda na kuwa raisi na Julai 10, 1993 aliapishwa na kuwa rais wa kwanza wa kuchaguliwa kupitia mfumo wa demokasia nchini Burundi huku akimteua Bi Sylvie Kinigi kutoka chama cha upinzani cha Uprona kuwa waziri mkuu. lakini miezi mitatu baada ya ushindi wa Ndadaye kupitia chama chake cha Frodebu. Ndadaye Melchior naye akapinduliwa na kikundi cha wanajeshi wa kitutsi mapinduzi yake yalitekelezwa kwa yeye kuuwawa na kufatia machafuko ya kimbali Burundi.

Kufatia hatua hiyo hatimae tarehe 21 Oktoba 1993 François Ngeze alichukua nafasi ya muda wakati taifa likishuhudia machafuko ya kikabila mpaka tarehe 27 Oktoba 1993, François Ngeze alitawala nchi ndani ya siku Saba tu na kumpisha mwana mama na aliyekuwa waziri mkuu wa Ndadaye Bi Sylvie Kinigi tarehe 27 Oktoba 1993 mpaka tarehe 5 Februari 1994, kwa muda wa miezi mitatu Sylvie Kinigi alikuwa raisi wa Burundi kama raisi mtendaji tu kwa kuipeleka nchi kwenye utulivu wa kitaifa.

Tarehe 5 Februari 1994 bunge likamuizinisha Cyprien Ntaryamira kuwa rais wa Burundi ambae alihudumu nafasi hiyo mpaka tarehe 6 Aprili 1994 pale Cyprien Ntaryamira alipo pata ajari ya ndege mjini Kigali akitokea Tanzania kwenye kikao cha upatanishi juu ya migogoro ya kikabila, ajali hiyo ilimpata yeye pamoja na raisi wa Rwanda kipindi hicho Juvenal Habyimana ambapo wote walipata ajari kwa ndege walio kuwa wamepanda kufatia ndege yao kutunguliwa na wote kupoteza maisha.

Kufatia kifo hicho Sylvestre Ntibantunganya aliyechukuwa nafasi kama rais kutoka kabila la kihutu ili kupoza machafuko yaliyo kuwa yameanza kutapakaa nchini humo lakini Ntibantunganya naye akapinduliwa na Pierre Buyoya tena mnamo tarehe 25 Julai 1996 mpaka tarehe 30 Aprili 2003 pale Pierre Buyoya alipo mpisha Domitien Ndayizeye kufatia makubaliano ya upatanishi.

Domitien Ndayizeye alitawala Burundi toka tarehe 30 Aprili 2003 mpaka tarehe 26 Agosti 2005 baada ya Domitien Ndayizeye kusaini mkataba wa amani na Arusha (Arusha Accod) uliomaliza machafuko nchini humo na hatimae tarehe 26 Agosti 2005 Pierre Nkurunziza kupitia Bunge la Burundi lilipomchagua kuwa rais kwa kipindi cha miaka mitano.

Tangu Nkurunziza achukue madaraka, hali ya amani ilipatikana Burundi, shughuli za kiuchumi zilifanyika bila mashaka yoyote, huku Wahutu na Watutsi wakishirikiana kuijenga upya nchi yao ambayo wao wenyewe waliibomoa kwa sababu za chuki za kikabila. Uchaguzi Mkuu 2010 ulifanyika kwa amani japo vyama vya upinzani vililalamikia kuchezewarafu lakini hakuna mtu aliyerejea msituni.

Ila kuelekea Uchaguzi Mkuu 2015, Burundi ilirejea kwenye machafuko tena. Mpaka sasa, zaidi ya watu 12,000 wanaripotia kupoteza maisha, huku tayari watu zaidi ya 250,000 wakiwa wameshaikimbia nchi yao. CNARED ilikuwa ni muungano wa vyama vya upinzani zaidi ya 20 nchini Burundi ambavyo viliungana kuhakikisha matakwa ya Katiba ya Burundi yanaheshimiwa, vilevile mwafaka wa mwaka 2000 uliosimamiwa na hayati Mandela. Kwa pamoja, CNARED wanampinga Nkurunziza wakimtuhumu kusigina katiba na kukiuka kile kilichoafikiwa kwenye mkataba wa amani wa mwaka 2000 jijini Arusha.

Hata hivyo tarehe 13 may 2015 yalifanyika mapinduzi mengine Burundi baada ya miaka 15 ya utulivu katika jaribio hilo liloshindikana rais Pierre Nkurunziza alikumbwa na jaribio la kupinduliwa, mapinduzi hayo yaliongozwa na kiongozi wa kijeshi aliyeitwa Meja Jenerali Godefroid Niyombare.

Godefroid Niyombare alitekeleza mapinduzi kwa kutoa taarifa siku ya jumatano majira ya saa nne asubuhi ya tarehe 13/5/2015 ambapo alitoa taarifa kupitia kituo cha radio cha Isanganiro kilichopo jijini Bujumbura huku akisema kuwa "Serikali ya Nkurunziza imevunjwa na jeshi limechukua nchi".

Niyombare alitekeleza mapinduzi kwa kusema kuwa wananchi wa Burundi wamepinga hatua yake Nkurunzinza ya kuwania muhura wa tatu. Japo mapinduzi hayo yalishindwa na serikali ya Burundi ilidhibiti tena nchi na serikali.

Huyu Jenerali Godfroid Niyombare alikuwa ni askari muhimu katika serikali ya Nkuruzinza aliyekuwa na madaraka ya juu jeshini na alikuwa ni mkuu wa Kitengo maalumu cha ujasusi nchini Burundi, ambaye serikali ya Nkuruzinza ilimfukuza kazi kama mkuu wa ujasusi mwezi februari miezi mitatu kabla ajatekeleza jaribio la mapinduzi.

Kufatia hali hiyo hali ya kisiasa nchini Burundi imekosa utulivu wa kitaifa, mapema mwaka 2018 ulifanyika mchakato wa mabadiliko ya katiba kwa kuongoza muhura wa raisi na kuongeza kipindi cha rais kwa kurefushwa kutoka miaka 5 mpaka 7 pamoja na mabadiliko mengine katiba mpya ilitoa mamlaka mengi kwa rais. Hadi sasa bado ustawi wa Burundi katika nyanja za kisiasa, kiuchumi na kijamii bado ayajarejea kwenye mustakabali wa kitaifa.

Pamoja mambo katika taifa la Burundi kurejea kwenye utulivu wa kawaida lakin wachambuzi bado wanaitazama Burundi kama moto unafuka Moshi hivyo wakati wowote unaweza kulipuka na kuwaka tena.

Kupitia historia ya mapinduzi ya taifa hilo huko nyuma unaweza kuona ni namna gani Pierre Khuruzinza yupo kwenye kibra wakati wowote ule ni nyakati tu inasubiliwa.

[emoji117][emoji420]Ukinakili kazi zangu kumbuka kufanya acknowledgment.

[emoji2400]Wako Mjoli wa Historia ya ulimwengu na diplomasia ya dunia......

Email- mbwanaallyamtu990@gmail.com

IMG_20190510_220434_953.jpeg
 
Kuhusu Nkurunziza naungana na kauli ya umoja wa Ulaya kwamba si rais sahihi wa kuivusha Urundi katika changamoto zake za kisiasa na kiuchumi
 
Tumeona tatizo la ukabila linasababisha janga kubwa sana kwa taifa?
 
Back
Top Bottom