MBOKA NA NGAI
JF-Expert Member
- Jan 31, 2025
- 350
- 576
Jeshi la Burundi limekanusha ripoti kwamba lilihusika na mashambulizi ya Mabomu huko Bukavu, Kivu Kusini, ambako mkutano wa AFC/M23 ulikuwa unafanyika.
Brigedia Jenerali Gaspard Baratuza, Msemaji wa Jeshi, amethibitisha kuwa hakuna Mwanajeshi wa Burundi ambaye yupo katika mji wa Bukavu.
Hilo linakuja baada ya Kiongozi wa M23, Bertrand Bisimwa, kupitia akaunti yake ya X, akisema kuwa baada ya uchunguzi, ilibainika kuwa vilipuzi vilitumiwa na jeshi la Burundi Mashariki mwa Congo.
Soma Pia: Waasi wa M23 Wateka Bukavu, Jiji la Pili kwa ukubwa Mashariki mwa DRC
Kiongozi wa M23, katika nyaraka zake, anathibitisha kwamba waandalizi wa kitendo hichi cha kigaidi, walinuia kumuua Kiongozi Corneille Naanga ambaye tayari alikuwa katika sehemu hiyo.
Watu 11 waliuawa na wengine 65 kujeruhiwa. Corneille Nangaa, anayeongoza AFC/M23, alikuwa tayari amewaambia washiriki kwamba ndani ya saa 48 wangewatambulisha Magavana wapya wa jimbo la Kivu Kusini kwenye maeneo wanayodhibiti na jiji la Bukavu.