Burundi yatangaza kufunga mipaka yake kuanzia kesho kutokana na Covid 19

Burundi yatangaza kufunga mipaka yake kuanzia kesho kutokana na Covid 19

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Serikali ya Burundi imetangaza kuwa itafunga mipaka yake ya majini na ardhini kuanzia Jumatatu ijayo, ili kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona ambayo yameonekana kuongezeka wiki hii.

Hatua hii imekua, baada ya wiki hii watu zaidi ya 40 kuambukizwa virusi hivyo ndani ya siku mbili katika nchi hiyo ya Afrika ya Kati.

Aidha, serikali nchini humo imetangaza kuwa abiria wote watakaowasili nchini humo kwa ndege, watalazimika kukaa karatini kwa muda siku saba na watakaopatikana na virusi hivyo, watapelekwa katika vituo maalum kwa gharama zao.

Agizo hili jipya limetolewa na Waziri wa usalama Gervais Ndirakobuca, wakati huu nchi hiyo ikiwa na maambukizi 884 ya corona tangu kisa cha kwanza kilichoripotiwa mwaka uliopita.

Hata hivyo, wadadisi wa mambo wanasema kuwa huenda nchi hiyo ikawa na maambukizi makubwa kinyume na inavyoripotiwa wakati huu kutokana na idadi ndogo ya upimaji wa virusi hivyo.
 
Kwa mambo na mwenendo kama huu tunaweza kusema sisi hapa kwetu hakuna maaambukizi kabisa?
 
Washirika wetu wa kubishana na uwepo wa korona wanazidi kutukimbia tu. Sijui nasi tutabaki na msimamo wetu hadi mwisho? Au Muheshimiwa Rais atutangazie siku zingine 3 za maombi kukabiliana na wimbi la mlipuko la pili hili. Muheshimiwa Rais, the sooner the better!
 
Hhahahah Burundi bhana sasa imehamia Afrika ya kati baada yakuona Afrika Mashariki haipati heshma stahiki
 
Wachezaji wa Simba kila mara na Barakoa
 
Back
Top Bottom