Busati la Mtoro

Busati la Mtoro

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
BUSATI LA MTORO

Nashindwa kufikiria nini kitakuja baada ya Busati la Mtoro.
Msikiti umejaa.

Watu wengi wamekuja wamejazana kusikiliza darsa.

Busati linawazungumzaji mabingwa wa fani zao kuanzia masheikh hadi madaktari bingwa wa maradhi ya binadamu.

Darsa hili linatazamwa katika televisheni kupitia ZBC 2 likirushwa mubashara na AZAM.

Kiongozi Mkuu wa Busati la Mtoro ni Sheikh Abbas Ramadhani Abbas mtoto wa Sheikh Ramadhani Abbas.

Baba Sheikh na mtoto ni Sheikh na ndiye Imam wa Msikiti wa Mtoro.

Naogopa kukisia ni watazamaji wangapi wanakiangalia kipindi hiki Busati la Mtoro.

Kurusha kipindi mubashara saa moja gharama yake ni milioni 15.
Vipindi hivi hufanyiwa marudio na vipindi hivi vyote hulipiwa.

Nashindwa kukisia gharama.

Ndani ya Msikiti wa Mtoro juu kuna chumba cha "crew," waendeshaji wa mitambo zaidi ya 10 kuhakikisha kipindi kinakwenda hewani sawasawa.

Hili ndilo Busati la Mtoro.

Allah laiti atamwonyesha huko kaburini Sheikh Mtoro Mwinyimangara darsa hili la Busati la Mtoro ndani ya msikiti alioasisi hakika atatatazika.

Sheikh Mtoro Mwinyimangara amefariki ameacha msikiti mdogo sana.

Naamini haikupata kumpitikia hata kwa mbali kuwa msikiti ule mdogo alioucha utakujakuwa msikiti mkubwa wa kutajika katika misikiti mikubwa ya Dar-es-Salaam.

Ilikuwa katika miaka ya 1970 ndipo misikiti mingi ya Dar-es-Salaam ilianza kuvunjwa na kujengwa upya.

Mmoja wa misikiti iliyojengwa upya ulikuwa Msikiti wa Mtoro.
Naukumbuka vyema msikiti huu mpya.

Kivutio kikubwa cha Msikiti wa Mtoro mpya ukitoa vipaza sauti katika minara ya msikiti yalikuwa mabomba ya maji kwa ajili ya kutawadha na mabusati ndani ya msikiti.

Mabomba ya kutawadha yalikuwa mengi na msikiti ulikuwa na nafasi kubwa ya kusali kwa wanawake na wanaume.

Darsa ya tafsiri ya Qur’an iliyokuwa ikisomeshwa na Sheikh Abdallah Chaurembo limeacha historia ya pekee.

Ilikuwa kama vile darsa lile la tafsir ya Qur’an linajenga msingi wa baadae ndani ya Msikiti wa Mtoro kuja kusimama Busati la Mtoro.

Naamini wakati ule hakuna aliyewaza kuwa pale katika Msikiti ule wa Mtoro utakuja kujengwa msikiti mkubwa na wa sifa na ndani ya msikiti huu patatandikwa busati la ilm - Busati la Mtoro.

Said Salum Bakhresa akauvunja msikiti huu na akajenga msikiti tulionao hivi sasa ambao sifa zake sote tunazijua.

Kubwa lililofuatia katika msikiti huu wa sifa wa Msikiti wa Mtoro ni hili Busati la Mtoro.
1712978949093.jpeg

 

Attachments

  • 1712679017724.png
    1712679017724.png
    1.7 MB · Views: 10
  • 1712679486748.png
    1712679486748.png
    3.4 MB · Views: 11
Back
Top Bottom