Bushoke na mapenzi yake kwa Papii Kocha

Bushoke na mapenzi yake kwa Papii Kocha

Ngaliba Dume

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2010
Posts
1,710
Reaction score
3,681
Miongoni mwa wanamuziki ninaowakubali ni Bushoke mwana wa Maxmillan(?)..sauti na idea zake mara nyingi huleta burudani kwa msikilizaji..Moja katika nyimbo zake nzuri ni "Msela jela",wimbo ulioimbwa maalumu kwa PAPII KOCHA WA BABU SEYA....Wimbo huuu ulitolewa mwishoni mwa mwaka 2005,naweza nisinukuu mashairi kwa ufasaha

"Ilikuwa J'pili 9/2 ama hakika siku ya visitors,mmemisi msela wangu maskani yetu Sinza,nimekwenda
kumcheki msela jela.... nimebeba mazagazaga kibao....amenipa kweli juu ya kesi yake
naongea kwa uchungu huku nalia,watu wanaimiliki kesi yake,vile anawapa "hi".vile anawasabahi
,nilipomwona kwa mbali nilifurahi...alipofika karibu I started
to cry...Msela amechoka..msela amaekonda...ana mapere mwili mzimaaa...msela kanambia yeye hakukosa,
ila tu ushahidi haukutosha,Tumuombee msela atatoka,japo ataanza maisha mapya hiyo si kitu il mradi
katoka.....weyoo weyooo weyooo...tumuombee msela atoke...mammmaaiii mammmaaaaiii...hata kama
nikifa P atoke hata kwa msamaha wa Rais....Rais mtoe P watu wanampenda P...Rais mtoe P.........
watu wanamtaka P
........

Kwa anaefuatilia mziki,huu wimbo ulitolewa kabla ya uchaguzi mkuu wa 2005,Mgombea fulani wa CUF jimbo la Nyamagana 2005,somebody Mbalamwezi a.ka. "Homa ya Jiji" ALIUTUMIA SANA na wafuasi wake nyakati za mwanzo za kampeni,baadae kwa ghafla sana Bushoke alijumuishwa katika kundi la wanamuziki waliozunguka na mgombea wa CCM Tz nzima,akifuatana na Komba,Wanaume na Vicky Kamata...Bushoke alibadili wimbo wake wa "mume -----" na kuisifia CCM...Baadae wimbo huu wa "Msela Jela" ukapotea kabisa ktk vituo vya radio...haukupigwa tena...wimbo ambao mpaka leo Papii akiwa gerezani hupenda kuusikiliza..mana huumpa matumaini...nimekumbuka hii sbb nilimtembelea mda flani.na Papii akauulizia...akaomba watu waendeleee kuomba ktk vituo vya radio ktk vipindi vya chaguo la msikilizaji...labda Rais aweza kumpa msamaha toka kifungoni kabla hajamliza muda wake..."Rais mtoe P..Watu wanampenda P"
 

Attachments

  • BUSHOKE.jpg
    BUSHOKE.jpg
    49.7 KB · Views: 271
  • PAPII.jpg
    PAPII.jpg
    22.5 KB · Views: 281
Mkuu, unaposema atolewe kabla ya muda wake unamaana gani? au haujui kua amefungwa kifungo cha Maisha?
 
Mbakaji aachiwe while ushahidi na manii yao yalipatikana kwa watoto wadogo..

Wangekuwa wanao ungalisema hivi
 
Back
Top Bottom