Business development unit ndani ya Serikali

Business development unit ndani ya Serikali

Ichwampaka

Senior Member
Joined
Nov 19, 2018
Posts
145
Reaction score
118
KUANZISHA BUSINESS DEVELOPMENT UNIT (BDU)

Kuungwa Mkono

Pongezi nyingi sana kwa serikali kwa mambo makubwa yanayoendelea kufanyika nchini. Hayahitaji hata kutangazwa kila mtu anaona na kusikia hata kuyagusa kwa mikono. Viva Rais John Magufuli kwa uongozi thabiti na wenye malengo. Kuna umuhimu wa watendaji kuwajibika zaidi kwa kutimiza wajibu maana tuna Rais ambaye anaweza kusikiliza, kushauri, kutoa maamuzi haraka na kusimamia mambo yakafanyika. Mimi nashauri kuanzishwa kwa kitengo cha uanzishwaji wa fursa mpya za kimapato ya serikali (revenue generating streams) katika serikali kuu.

Kubadili Mtazamo
Idara, Mamlaka, na Vitengo vya Wizara waondokane na fikra za kutegemea ruzuku tu bali kuangalia namna ya kutengeneza fursa za kuzalisha mapato ili kuongeza tija na ufanisi wa utoaji huduma. Wakifanya hivyo, bajeti zao za OC zinaweza zisitokane na ruzuku, bali kwa mapato yao ya ndani. Na vitengo vingine vinaweza kutimiliza kwa 100% utoshelevu wa kiundeshaji (operational Self Sufficiency).

BDU haitakuwa sehemu ya kutengeza sera, urasimu au uraghibshi, hapa ni maalumu kwa ajli ya kutengeneza mapato ya serikali basi. Sio kuendesha warsha, makongamano, semina…..BIG NO. Tutaenda mahali ambapo tunatengeneza fursa kumbuka BDU itakuwa inajiendesha kwa mapato yake yenyewe baada ya kupeleka mapato hazina. Miradi mingine itakuwa ya muda mfupi, tukishaanzisha itaendelea yenyewe, mingine tutaendelea kuisimamia. Wazo kuu ni kwamba wawepo watu wachache (vichwa) wanaofikiria kila siku jinsi ya serikali kuongeza mapato yake.

Wapi Tunaanzia
Kwa leo nianze na kazi BDU inaweza kufanya ndani ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Kwasasa mapato ya serikali yanategemea vyanzo vile vile vya siku zote na vingine vimepungua kutoka na kukosekana kwa ‘dili’, upigaji haupo tena au sababu nyinginezo. Kupanua wigo wa walipa kodi (Broadening tax base) na kurefusha kina cha walipa kodi (deepening tax base) ndio njia kongwe zinakubalika katika kuongeza ukusanyasaji wa kodi. Kitengo hiki kitatumia njia zote mbili ingawa kwa kiasi kubwa zote zimekuwa saturated mpaka uwe na jicho la tai.

Kutanua Wigo wa Walipa Kodi (Broadening Tax Base)
Kundi la kwanza
Ni watu wanaofanya shughuli endelevu zinazoingizia mapato ya uhakika lakini hawajasajiliwa kuwa walipa kodi. Hao watasajiliwa rasmi na TRA, zaidi ya hayo BDU itawasiliana na mamlaka husika na aina ya hiyo shughuli ili waweze kupatiwa utambulisho wa kipekee (exclusive rights) kufanya shughuli hizo. Mchakato wote huo utafanywa na BDU, mteja atapatiwa vyote hivyo katika dirisha la BDU (one stop center). Hakuna gharama zaidi ya kusajiliwa na TRA ambayo ni bure, kazi yake itakuwa ni kulipa kodi tu.

Kundi la pili
Kuna watu wanaofanya biashara ambazo ni endelevu (sustainable) na zinafanya vizuri kimapato lakini kulingana na mfumo wa utendaji wa TRA ni vigumu mno kuwasajili watu hao kama walipa kodi, yaani ni ngumu kwa TRA kuwafikia. BDU itazifikia hizi biashara popote zilizopo. BDU itatoa elimu ya kodi, elimu ya kutunza kumbumbuku za biashara, umuhimu wa kulipa kodi, kisha itawasajili rasmi na kuwaingiza kwenye GPS ili kuwa na coordinates kwa kila biashara. Kwa zile biashara mpya, kivutio kuingia katika mpango huu ni kuwa ukisajiliwa chini ya huu mpango, hulipi leseni ya biashara wala vikorokoro vingine vyote. Hivi vyote vitalipwa na BDU na utachukua vyote siku moja kwenye dirisha moja la BDU (One stop Center)

Kundi la Tatu
Kurasmisha biashara zilizo chini ya kundi la ujasiliamali zinazotumia vitambulisho maarufu kama vitambulisho ya Rais John Magufuli. BDU itahusika na mpango wa kuwa transition hawa wajasiliamali kutoka hatua hii kuingia kwenye wigo wa kuanza kulipa kodi. Vitambulisho vya ujasiliamali ni daraja la kuwavusha kuingia hatua nyingine ya kutambulika rasmi. Rais alishatoa dira ni muhimu kuwe na mwendelezo wa maono ya Rais kuhakikisha kila mtanzania anapata nafasi ya kufanya ujasiliamali bila kubughudhiwa.

Kivutio kuingia katika mpango huu ni kuwa ukisajiliwa chini ya huu mpango, hulipi leseni ya biashara wala vikorokoro vingine vyote. Hivi vyote vitalipwa na BDU na utachukua vyote siku moja kwenye dirisha moja.

Kundi la Nne
kusambaza vitambulisho vya ujasiliamali kila mwaka kwa wajasiliamali wapya wanaoingia katika sekta. Kila mwaka kuna fursa mpya za ujasiliamali, pia kuna wanafunzi wanaohitimu katika shule na vyuo mbalimbali. Hivyo, zoezi la utoaji wa vitambulisho litakuwa endelevu, na pia kuhitimu kuingia hatua ya pili ya kutambuliwa rasmi pia litakuwa endelevu. Biashara yoyote lazima ikue au ife, huwezi ukawepo halafu ukawa hukui

Kurefusha Kina cha Walipa Kodi (Deepening Tax Base)
Kuna kundi kubwa la wafanyabiashara ambao wanalipa kodi isiyo stahiki (mara nyingi wanalipa chini ya kiwango). Lakini pia kuna kupishana kwa kanuni ya ulinganifu wa mlalo (The principle of horizontal equity) hii pia inahitaji kuangaliwa (sitaweza kuongea zaidi hapa kwasababu nitakuwa naongelea utendaji wa sasa wa Mamlaka).

BDU itakavyofanya Kazi
Kitengo hiki kipya kazi yake kubwa itakuwa kusajili vyanzo vipya vya kodi, hawa watakuwa watu wa nyanjani (field) 100%. Watu walioko ofisini kazi yao kubwa itakuwa ni kuchakata na kukadiria kodi. Kwa jinsi ilivyo sasa, Afisa wa TRA akikaa ofisini kwake yuko busy kuhudumia wateja muda wote wa kazi, ni ngumu sana kupata wasaa wa kufikiria vyanzo vipya vya kodi au kwenda nyanjani kutembelea wateja ispokuwa kwa suala maalumu, muda mwingi wametingwa na paper trails kuanzia maafisa mpaka viongozi wa ngazi za juu. Ni sawa na nurse au tabibu hana muda wa kufikiria juu ya njia mpya za kimatibabu yeye yupo busy kutibu tu. Lakini hata katika viwanda kuna vitengo vya utafiti na maendeleo (Research and Development) vinavyofikiri juu ya ubunifu wa huduma mpya.

Kitengo hiki kitafanya kazi kwa matokeo (results based). Mfano, wilaya ya Ilala yenye kata around 23 kuanzia 1st July 2020 hadi 30th June 2021 inatakiwa kusajili walipa kodi wapya 2,000 ambao kwa wastani kila mlipa kodi alipe Tsh 1,200,000 kwa mwaka, mapato yatapatikana Tsh 2.4b. Gharama za uendeshaji za juu kabisa (42%) inaweza kuwa Tsh 1,008,000,000, hivyo serikali kubakia na Tsh 1,392,000,000. Hapa inaweza kuwa kwa wafanyabiashara wale ambao tayari wanafanya kazi au kwa wale ambao wanaanza biashara (start ups).

Hapa nimetolea mfano kwa wilaya moja tu, unaweza kuona kama utaratibu huu ukifanywa kwa nchi nzima. Tunaweza kuanza kwa majaribio mikoa michache tutahitaji serikali iikopeshe BDU kwa ajili ya bajeti ya kuanzia lakini baadaye BDU itailipa serikali. Hiki kitengo kitajitegemea kwa kila kitu kwa maana ya gharama zake sio kutegemea ruzuku.

Baada ya hapo kitatanua shughuli zake na kufanya process mapping katika idara na mamlaka za serikali ili kuona mianya ya urasimu katika serikali inavyochangia serikali kupoteza mapato yake. Mfano, ni wizara ya viwanda na biashara hasa kitengo cha utoaji wa leseni na usajili wa makampuni, kujaza ritani za kila mwaka na ufutaji wa makampuni. Hapa pia kuna mabilioni tunayokosa kwa kukosa ubunifu mdogo na kushindwa kubadilisha mentality.

Kuna vitengo kama usambazaji wa pembejeo za kilimo. Hii ni sehemu nzuri sana ya kutoa huduma lakini pia kutengeneza mapato ya serikali. Serikali itamkomboa mkulima kwa kuuziwa pembejeo duni, kwa bei kubwa na kwa wakati usiofaa.

Kuna Wakala wa Kuteneneza magari ya Serikali. Shida iko pale ni mentality na attitude hata ukiajili mainjinia wawe watu wa procurement sio suluhisho. Tatizo wanaelewa kuwa wao wanatakiwa kuwa revenue generating centers na sio cost centers? Kwamba mishahara yao 100% itatokana na utendaji wao?

Pita kwenye ofisi za serikali uone mashine, vifaa, magari, mitambo inavyooza utalia machozi. Nilijaribu kuuliza idara moja niliona Pick Double Cabin imekuwa grounded zaidi ya miezi sita kwa sababu ya side mirror moja. Ukiulizia kwanini mali za umma zinaachwa zioze utaambiwa mali ya serikali haina mwenyewe au utaambiwa taarifa ilishapelekwa kwa mthamini mkuu wa mali ya serikali unasubiriwa uratatibu. Utaratibu gani huo wa kupoteza mabilioni ya fedha. Kama hayo mavitu hayatengenezeki, BDU ikabidhiwe kwa amri ya Rais yauzwe na hizo fedha akabidhiwe mtu ambaye watanzania wanamuamini kuwa anaitendea haki hata senti moja wanayomkabidhi ili ajenge miundombinu kama alivyoahidi juzi akikagua maendeleo ya ujenzi wa Ubungo interchange.

Mambo mengi Rais wetu anafanikiwa kwasababu yeye ameusoma ‘mchezo’ muda mrefu alivyoingia madarakani anafanya tofauti na watu wengi walivyozoea na walivyokuwa wanatarajia rais kufanya. Ndio maana wengine wanashangazwa na baadhi ya maamuzi, hotuba na utendaji wa Rais. It is all about changing mentality and attitude.

Serikali inahitaji watu wenye the right attitude na skills kufanya haya, watu wanaotazama mambo kwa jicho la pili. Na uzuri watu hao tupo na pacesetter (Rais John Magufuli) yupo, hakuna kinachoshindikana ni kubadilika tu kuachana na ‘’Business as usual’’.

Nitume mimi Bwana, nipo tayari kutumika.

tunatekelezam@gmail.com
 
Back
Top Bottom