Business Idea! Drop your comment

Dr wa Kaliua

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2020
Posts
1,634
Reaction score
3,833
Habari JF

Mimi kama mwanafunzi wa chuo kikuu, leo hii nimeamua kuwasaidia wanafunzi wenzangu kwa kuwapa mpango mzuri wa biashara.

Usishangae sana, uzuri? Wa mpango huu wa biashara unaweza kuanza bila mtaji kabisa. Yaani ukaanza kwa uwezo wako mzuri wa kufanya mawasiliano kupitia smartphone yako.

Kupitia uwezo wako wa kuongea na kuhamasisha.
Kwanza naanza kwa kukupa tatizo na jinsi ya kusolve.

Twende champion!
Hivi umeshawai kwenda mahali hapa dar es salaam, ukakuta hakuna huduma muhimu kama maduka mpaka ukajiuliza hivi hawa watu huwa wananunua wapi nyanya?? Karoti?? Bamia nk??

Nina imani umeshawai kuona jamii ya namna hivyo, mara nyingi maeneo ya hivyo yametawaliwa na high na middle class..yani watu wa hali ya juu na kati wengi ni matajiri..na kuna wale wa tabaka la kati .

Sasa unachotakiwa kufanya wewe ni kusambaza huduma.hakuma kitu anapenda binadamu kama kuonekana wa thamani hata kama hana kitu.

Sasa unaweza kufanya biashara nyingi, ila leo naanza na hizi fast moving product yaani bidhaa zinazotembea na kutumika kila siku.

Usishangae sana.
Hapa unaenda kuanzisha kitu kinaitwa Mobile Genge, au genge la mtandao.

Unachokifanya wewe, ni kwenda nyumba hadi nyumba kuomba order juu ya maemezi ya kesho..

Dili na vitu common kama nyanya, viazi, ndizi, pilipili nk.
Baada ya mtu kukupa order wewe unaenda ilala kuchukua mzigo limited kutokana na watu wali request aisee utapiga pesa balaa. Na hutokuja kupata hasara

Ukimaliza kuwa karibu na wateja wako utaunda kikundi cha whatsap kila mteja atatoa oda yake humu..

Mambo ya kuzingatia
Kila nyumba utakayo toa huduma hakikisha ni nyumba ya kishua kuna fense kali yani kwa madoni, wao wanapenda kuletewa.

Hakikisha unamuelezea mteja wako vizuri akuelewe na ahitaji bidhaa yako usiforce...

Komqa baadae tafuta usafiri wako, ukiwa vizuri nunua toyo unanunua vitu then unatembeza kwa wateja wako wanachagua

Naendelea vizuri kwa sasa.
Maoni yote yanaruhusiwa wazeee wa kutukana uwanja ni wenu.
 
Hawa madon si ndio wanaendaga shopping wenyewe? Hadi nyanya wananunua supermarket?

Ila wazo zuri.
Yani supermarket wanafata
Hapa unawapelekea kwao you see??

Yani nasemaje naseeemaje hii Idea tamu sana.
 
Ni ushauri mzuri ila si mzuri sana kwa mwanafunzi, kwa biz hiyo muda ndio mtaji wako, na muda ndio huo unauhitaji chuo.
 
Ni ushauri mzuri ila si mzuri sana kwa mwanafunzi, kwa biz hiyo muda ndio mtaji wako, na muda ndio huo unauhitaji chuo.
Mkuu ukishapata angalau wateja kumi wa kudumu
Unaweza kuajili vijana.

Kazi yako inakuwa kufuata mzigo pekee alafu madogo wanasaply
 
Is not easy to understand this son but hope if u try it u will come back with different experience.
 
Habari JF

Mimi kama mwanafunzi wa chuo kikuu, leo hii nimeamua kuwasaidia wanafunzi wenzangu kwa kuwapa mpango mzuri wa biashara...
Hela utapata vipi hapa Bado sijakuelewa , hebu fafanua nikishampelekea nyanya mm nanufaikaje
 
Hela utapata vipi hapa Bado sijakuelewa , hebu fafanua nikishampelekea nyanya mm nanufaikaje
Okay
Nyanya wewe unanunua kwa jumla then unauza rejareja

Yani mkuu hili ni genge ila tofauti ipo kwenye order na delivery
Wewe unanunua kwa idadi maalumu na watu maalumu.
Ni ngumu kupata hasara.

Mimi nimewaifanya kazi ilala sokoni, ahsubui nyanya za 1500 huku mtaani ni 3000 nakuendelea.

So cost yako itakuwa juu kwani unajumlisha na gharama ya usafiri.
 
Nimekupata
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…