Moaz
Member
- Apr 6, 2018
- 88
- 127
Business idea hii itabase kwenye moja ya sehemu yenye idadi kubwa ya watu ukiacha mziki nayo si nyingine ni Soka(Mpira wa Miguu). Soka letu linakua kiasi sasa ni muda wa kutumia fursa mbalimbali zilizopo kwenye Soka.
Je ni ipi hiyo business idea?
Hii ni business idea kwa ajili ya kuanzisha jukwaa la mtandaoni (Online platform) la mchezo wa mpira wa miguu. Jukwaa ambalo litawakusanya wadau wote wa mpira wa miguu nchini kuanzia Makocha, Walimu, Wachezaji, Wachambuzi, Viongozi na Waandishi wa Habari.
MALENGO MAKUU
1-Kutoa na kushare elimu ya mpira miongoni mwao.Ni wazi kwasasa Tanzania tunahitaji jukwaa ambalo tutazungumzia maswala ya kiufundi Zaidi kwa ajili ya kuinua na kukuza elimu ya mpira kwa wadau wote nchini kuanzia kwa wachezaji chipukizi hadi kwa makocha wazawa.
2-Makocha wetu kushare mawazo yao ya kiufundi zaidi hii itawasaidia kuongeza uelewa wao na kupelekea kuwa na ushindani wa kimbinu na Kifalsafa zaidi kwa makocha wetu wazawa.
3-Uchambuzi wa kiufundi zaidi utakao tolewa na wadau mbalimbali kimbinu zaidi.
4- Chanzo cha elimu kwa vijana wetu wanaochipukia. Kutakuwa na Education articles mbalimbali ambazo zitaongeza football intelligence yao hivo kuinua vipaji vyao katika njia sahihi.
5-Kupeana Story za wakongwe pamoja na kupata busara zao.
6-Mashabiki kupata maarifa ya kuutambua mchezo kitaalamu na kwa kina na sio kihisia na kishabiki tu hii itaongeza ladha ya mchezo wa soka Nchini miongoni mwa mashabiki
Hizo ni sababu chache katika nyingi ambazo ninahakika ni zenye manufaa makubwa katika ustawi wa mpira wetu Tanzania.
Kwanini Online Platform kuhusu mpira?.
Kuwa na Platform ambayo itakuwa full package katika soka ni hatua muhimu kwa sasa kwa kuwa itatimiza Malengo husika pasina kuwa na distraction zozote. Kwa kuwa watu watakuwa wanaongea mpira tu.
Ni wazi kama taifa tumejaaliwa vipaji vikubwa sana changamoto ni kuwa vipaji vingi vinashindwa kufikia mafanikio makubwa kwa kukosa elimu ya msingi ya mpira (Football education). Taifa letu lina idadi kubwa wanamichezo ambao wanahitaji kupata elimu ya msingi ya mpira wa miguu kwa namna yeyeto ile, kutokana na changamoto za miundombinu ambalo lipo nje ya uwezo wetu jamii kubwa bado haziwezi kupata elimu ya mpira kwa urahisi na wakati sahihi.Hivo inatulazimu tutumie fursa ya Technology kuweza kutatua tatizo hili.Wachezaji wengi wanafika hadi kucheza Ligi kuu wakiwa hawana elimu ya msingi ya mpira(Technical,tachical na Psychological) hii inatupunguzia sifa ya kuweza kupata wachezaji wenye profile za kucheza mpira wa kimataifa hata kama tunavipaji kiasi gani kutokuwa na elimu inawaondolea sifa ya kuwa wachezaji professional ukizingatia tumo kwenye miongoni mwa ligi bora barani Afrika.
Jukwaa la kimichezo lenye Wataalamu katika kila idara litachangia maendeleo makubwa ya mpira wetu kwa kuwa wataalamu hao watatoa elimu hiyo na kuweza kuwafikia watanzania wengi nchini. Tunafahamu uwepo wa internet ndio huduma pekee ambayo imesambaa kwa eneo kubwa nchini. Hivo jukwaa hilo litakuwa ni chachu na muongozo kwa wanamichezo ambao hawapo kwenye mikoa yenye miundombinu na pia waliopo kwenye hiyo mikoa watanufaika kwa kuongeza ujuzi Zaidi.
Najua ipo mitandao ya kijamii ila mitandao takribani yote ipo kwa ajili ya kuripoti habari za kimichezo. Sina uhakika kama kuna platform ambayo inatoa huduma ya elimu ya mpira online.
So ni idea ambayo ni kubwa na inahitaji watu wenye maono makubwa watu ambao wanaona fursa kwenye idea na walio tayari kuleta mabadiliko na maendeleo katika jamii.Kwa yeyeto atakaye kuwa tayari tuweze kudiscuss na kuweza kuangalia tunaachaje athari katika jamii yetu mlango uko wazi karibu.