[QUOTE=Kassamali,
Mkuu.Kuna watu wengi tu wenye mapesa yao kibao mfukoni km wewe lakini hawajui wayafanyie nini, matokeo yake ni kiungia mkenge.Ndg yangu Kassamali kimsingi wazo lako la kuwekeza pesa zako sio baya ni zuri tu, ila mbinu unayotumia kutafuta huo uwekezaji sio mzuri sana, kwa kama Babalao alivyosema hapa Bongo matapeli ni wengi tena wanajua sana kupanga mipango, wabunifu kweli kweli, waandishi wazuri sana wa michanganuo ya kibiashara, wacheshi,wakarimu mno, wapole, lakini mwisho wa siku wanakuacha pabaya.
Ndg yangu sauala la kuwa partnership na mtu usiyemjua vizuri kabisa ni hatari sana ktk ulimwengu wa kibiashara, ushirika ktk biashara ni mgumu mno unataka mtu ajitoe kikamilifu,awe muwazi,awe na nidhamu, awe mkweli, mpenda haki, awe muelewa, mwenye maono pia akubari kuwajibika bila kinyongo.sifa hizi watanzania wengi hatuna.
tumezoea kufanya mambo kiujanja ujanja tu, kiusanii au kwa lugha ya kisasa tumezoea kuchakachua kila jambo.
Ndg yangu jaribu kutafuta wazo, kisha fanya wewe mwenyewe,cha mhimu ni kuwa na timu nzuri ya watu wa kukushauri juu ya wazo husika,pia katika kusimamia kazi.Lazima uwe makini sana na suala la Management kwani ndiyo mhimili wa kazi,ukilala hapo ujue imekura kwako.
Wasiliana na Babalao atakupatia mawazo mazuri tu,mie namjua hana shida ilimradi umuandalie vijisenti vya kupelekea watoto wake nyumbani.Mungu akubariki ndg Yangu.