Business ideas (Bure)

Mimi ushauri wangu ni mmoja tu, nenda Njombe au Iringa nunua kitalu cha miti, panda miti ya kutosha, tulia kama miaka 5 utaweza kuja kuvuna mara nne zaidi ya hiyo pesa, na hapo utakuwa umetengeneza kama faida ya uhakika ya Laki tano tu kila mwezi japokuwa faida yote utakuja kuipata mwishoni kabisa.

Kama hauwezi hiyo, basi nenda kanunue viwanja kwa bei rahisi maeneo ambayo bado hayajaendelezwa baada ya kuusoma mchezo vizuri, ukinunua hivyo viwanja viboreshe kidogo kimiundo mbinu halafu tulia kimya hata kama miaka Mitatu hivi, na hapo utakuja kuviuza kwa bei zaidi ya mara tatu uliyonunua na kuviendelea. (Hapo Faida ni kama Laki mbili hivi kwa mwezi, na tena utaivuna mwishoni).

Hakuna shortcut katika biashara.
Ukitaka makubwa sana na kama huna uzoefu wa biashara tegemea kuupoteza mtaji wote wa biashara ndani ya muda mfupi sana.
 
kaongeze elimu, kama una degree kachukue MBA.

kitendo cha ww kutojua biashara ya kufanya, ni kiashiria kuwa elimu yako inahitaji kuongezwa kidogo.
Hapo umempa wazo......hiyo ndio investment bora kabisa
 
Tuwe wakweli biashara ya miti ipo ktk orodha ya biashara ya kubett......Kuna jamaa alikuwa na ekari 5 vijana wakapiga moto zote...Pia sasa wameanzisha tabia mbaya sana mtu anakuuzia shamba la miti kumbe ameshakopea BANK.....baadae linakuja kuuuzwa na bank unaanza kulia.......
 
Kweli kabisa.Riba mbaya......Riba ni chanzo cha ufakiri.......ila wengi hawajui......ndio maana watu huuziwa nyumba zao au ufilisika baada ya kujiingiza ktk mikopo ya riba
 
Fungua kibanda cha kuuza supu ya pweza maeneo yenye vibosile wa kutosha.
 
Pia niliwaza kukopesha watu kwa riba, ila Enzi hizi nafikiri rejesho litakua ugomvi
Mkuu, kama wewe ni Mkristo (hauna tatizo na suala la Riba)...tafuta kikoba kilichosajiliwa omba kuwa mdhamini wao kwa makubaliano ya kupatiwa 10% au zaidi kwa kila mwezi. Hakikisha unapoingia katika makubaliano hayo unakuwa na mwanasheria wako ili msainishane mkataba na wateja wako. Ni biashara isiyo na stress kabisa. "Ukitaka kufanikiwa fanya biashara na masikini", hii ndio principle ya matajiri wote duniani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakushauri kama unawatu waaminifu kwahela hiyo fanya biashara yapesa yani m pesa, tigo pesa nairtel money kwamtaji huo tafuta center nzur nakuhakikishia utapiga faida nzuri sana tena wala usiwekeze yote hiyo hela weka milioni 6 zinatosha sana mimi ninakiofisi changu chahuduma hizo namtaji wangu hata milioni haufiki ila faida naingiza sio chini yalak mbili kwamwezi nikishalipa pango nahapo Wateja kibao wananipita kwasababu yamtaji mdogo ila ningekuwa nahata milioni mbili naamini ningekuwa naingiza sio chini yalaki 5 sasa sembuse milioni hizo ulizonazo yani naamini kwahela hizo unafungua ofisi mbili zamaana naungechanganya faida naamini ungepata hiyo nahata kama isipofikia hiyo naamini ingekaribia hata kama ingepungua nikidogo sana, ila changamoto yake niwafanya kazi waaminifu nawenye kujua mitego yamatapeli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hebu nifafanulie vizuri mkuu sikuijua hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…