Business ideas (Bure)


Cortunix, Kumsaidia kaka most of the time wanafanya ule mchanganuo wa ingredients ni food laboratory. Hao wanachambua na kukwambia % za kila kitu.

Kuhusu jee utabadilishaje maono ya die hard Watanzania ambao wanaona kama sio kutoka shamba sio fresh. Hapa dawa ni marketing and educate consumer. Kuandaa mchakato wa kuelimisha walaji, mfano ni kwenda kwenye alaiki za watu na kuweka meza na kuanza kuelimisha kwamba wewe huleti kitu kipya kwenye soko, bali unaboresha vilivyopo, wewe humyonyi mkulima bali unamfanikisha. Hapa marketing ndio mwanzo mwisho, na marketing nzuri ni smart marketing. Kumbuka kwamba tunawalenga wateja wenye uweleo kidogo.

Mkuu kwanza kujitahidi product yako ifike nchi za maziwa makuu, na kama inakubalika dar basi hizi nchi za maziwa makuu it wont be a problem. Kisha hapa lazima utengeneze mchakato wa kupartner na World Food Organization ambazo ziko msatari wa mbele wa kupambana na njaa. Kumba mjasilimali ana save time and reduce cost and your product does both.

Tutafute muda tuzungumze social media marketing strategy, Galleria Warfare Marketing tactics, na nyingine nyingi.
 
nilipobold umeniacha mambo gani matatu? machine inaitwaje?
Mambo matatu machine inayofanya ni moja, Kuondoa Backeria kabla ya Kupack, Kuondoa Hewa ndani ya Can na tatu Kuhakikisha hakuna hewa inayoingia ndani ya can. Machine : Automatic Food Canning Machine, Shantou Xinhu Canning Machinery Co., Ltd.
 

Thanks
 


Asante sana mkuu kwa mambo uliyoyaeleza naamini yatasaidia wengi kwenye suala la uelewa hasa start up business.
kwangu nimejipanga kufanya zifuatazo( bakery (Cakes,burger na Mini pizza), Ice cream, Mobile fast food and Food processing product)

  • Ideas nimezifanyia kazi almost 1 year now na pia nimekwenda training tofauti tofauti kuhusiana na biashara hizo na zote nime qualify kuzitengeneza kwa ubora na design tofauti.
  • Nimefanya utafiti pia wa cost halisi, sales na profit from daily up to Years.
  • Pia nimefahamiana na wazalishaji mabalimbali na kuelewa challenge wanazokutana nazo etc
  • Pia nitakuwa na product tofauti tofauti na wateja wa rika mbali mbali na location kulingana na wateja
  • Pia kwa package nimefanya utafiti kwa wazalishaji wa ndani nchini na wa nje kuhusiana na ubora wa vifungashio.
  • Na kwasasa nimeshainvest pesa za kutosha katika kupata eneo na kulifanyia marekebisho na liko tayari kuanza kazi, na baadhi ya mashine nimeshanunua
  • kwa suala la masoko pia nimeshafanya utafiti almost many part hapa dar es salaam
Ndio hayo mkuu mpaka sasa nimefanya na nina uhakika Hizi biashara nitafanya vizuri.( my email ni ubakery@yahoo.com)
 
Wakuu basi nimeprocess Jam just to show mfano. Nimefanya Leo in my kitchen.
Hii is good for 3 years. Kuna other process zijaonyesha kama kuseal lead na nyingine. But you have an idea how package can change the world.
 
Umetoa very good observation Mtanganyika. Packaging na ile genaral presentation ya bidhaa inatunyima masoko sana. Kwa mfano packaging ya maziwa ya Tanga fresh huwa inanishangaza sana. Iko vile vile, style ile ile miaka nenda miaka rudi. Inamaana huwa hatufanyi improvemt ya bidhaa zetu kulingana na feedback toka kwa wateja na soko kwa ujumla! Hatujawa agressive ktk ku compete kibiashara. Unakuta hadi toilet paper watz tunatumia zinazotoka nje sababu zakwetu ni sawa na vumbi tu hazifai hata muonekano wa nje hauvutii kuinunua!

Mfano halisi wa winners and losers. View attachment 114442

Do you see why we can't compete? Branding and packaging are the weapon of any successful business.
 
Ya kufyatua na kuuza matofali nayo inalipa

Mdogo wangu alipomaliza university alijaribu hii business ya matofali. Nilopo kaa chini na kuangalia namba zake hii biashara ina gross margin ndogo sana. I call it razor skin margin. Gross Margin of 10%.

Standard margin ni 40% before general expenses. Maana bei ya kuuzia toa gharama za utengenezaji salio lazima liwe 40% ya bei
 
Ndugu Mtanganyika, nashukuru kwa somo zuri, kwakua inaonekana mawazo haya umeyafanyia kazi vema nafikiri itakua vema kupunguza dukuduku kwetu kwa kutupa mchanganuo mzima, kwani aina za biashara zinapishana mgawanyo wa mtaji. Mashine ya kusaga na kukodi jengo <16M, lakini stock ya miezi 3 inaweza kua >10x16M. Lakini upande wa Mgahawa unahitaji stock ya ~wiki 1, ambacho kitakua kiasi kidogo sana <16M/10.
Natanguliza shukran kwa mawazo yako.
 


ndugu yangu umeleta mawazo mazuri sana, binafsi nimeshawishika na kuvutiwa sana na hili la kuosha magari, lubes na kadhalika ila nilitaka kujua hizo hydrolic jakes na vifaa vingine vinaweza kugharimu kiasi gani na pia huo mtaji mdogo unaouzungumzia ni wa kiasi gani ili na mim nione kama naweza kujiingiza huko
 
Mimi ni kijana ambaye nina uchu na biashara, sema wazo la kufanya biashara gan ndo ishu. Nlikua naomba kujuzwa ni biashara gan naweza fanya ambayo mtaji hautazidi 3m.:lock1:
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…