Business ideas (Bure)

Nadhani unaweza aanzisha kuuza nafaka hapo mtaani kwako.
 
Nakushauri fanya biashara ya kilimo inalipa sana tu, kwa ushauri zaidi ione taasisi moja inaitwa ansaf, nadhani wako posta mpya hapa dsm.
 
Chukua matatizo yanayowakumba hapo mtaani kwenu then jaribu kuyageuza kuwa mawazo bora ya biashara kwa mfano huwa unasumbuka sana kupata luku unaweza kuweka kibanda hapo uwe unauza hizo coz wapo wengi wanaotafuta huduma hiyo kama wewe na wasiipate. vile vile unaweza kuwa na biashara ya kununua nafaka kama mahindi kutoa sehemu yanapouzwa bei ndogo na uyauze maeneo ambayo upatikanaji wake ni mgumu hivyo hata bei pia zitakua juu na kupelekea kupata faida na kukuza mtaji wako ili mwisho wa siku uwe unanunua mahindi unayachakata na kuuza unga + pumba ambayo inalipa zaidi.

AHSANTE
 

My favorite post this month.
 

Inabidi tuangalie swala linaloitwa specialization of labor. Sio kila kitu ufanye wewe, fanya kile kinachokutoa na waachie wengine wafanye mengine.

Kwa mfano, utakuta mtu ameajiriwa na anakomaa na biashara nje ya ofisi, ofcoz lazima ile kwako. Kwasababu ili ufanikiwe kwenye biashara unahitaji commitment/dedication, hardworking, channeling. Utapata wapi hivi wakati upo kwenye ajira?
 
Pia tusisahau dhana ya kukuza biashara.

Usikubali hata siku moja biashara yako idumae. Utakuta mtu anaanzisha biashara inakaa miaka na miaka in the same location, the same size.

Kama unalima, sio kila siku unalima eka yako moja au mbili. Weka time frame within 10 years unatakiwa uwe na kama eka 100 unalima.

Kama una duka, basi komaa uanzishe super markets.

Biashara za siku hizi ni akili na channeling. Ujue unazalisha nini, unazalisha wapi, unamzalishia nani, unapeleka wapi, unapelekaje. Ukikaa kila siku unaamka na kurudi kulala unaenda ili mradi itakula kwako.
 
Mfano halisi wa winners and losers. View attachment 114442

Do you see why we can't compete? Branding and packaging are the weapon of any successful business.

Habari mtanganyika.

Upo sawa kabisa hasa kwenye packaging. Wengi wetu hatujui kuwa packaging ndo marketing tosha ya bidhaa yako. Na pia packaging ya wengi wetu ni kufuata mkumbo na si kukaa chini na kudesign anachotaka kitokee. Utakuta ndani kuna bidhaa nzuri sana ila imefungwafungwa ili mradi na yeye anauza.

Tuje kwenye marketing.
Kuna aina mbili ya marketing ambayo unaweza kuifanya hasa kwa canned foods. Ya kwanza ni ile inaitwa "nenda kamwambie mwenzako". Kwamba, unakuwa na targeted customers wa bidhaa yako. Tuseme unawatarget wale wanaotoka au wanashinda maofisini muda wote na hawana muda wa kwenda sokoni. Unakuwa na bidhaa zako tayari packed then either unapitisha maofisini au unafungua duka kwenye zile njia ambazo targeted customers wanapita. For this case kama nyerere road, sam nujoma au kawawa road. Hawa wakishatumia bidhaa yako wanaenda kuwaambia na wengine.

Nyingine ndo ile ya mass media, unatumia vyombo vya habari na social sites kuelezea bidhaa yako.

Eventually lazima bidhaa yako igain popularity endapo itakuwa na ubora ambao haumuathiri mtumiaji.
 
Wadau mmechangia mambo ya maana ni nimeanza kuyafanyia kazi soon nitakuja na wapi nime achieve na challange zipi nimeface ili wengine nanyi mfaidike pia
 
Mimi Nimefikiria Kuanzisha Mobile Phone Internet Cafe,nitakachokifanya Nanunua Smartphone 5 Au Kumi Zakuanzia Kisha Natega Huku Uswazi Wengi Hawajui Kutumia Computer Ila Cm Wanajua Pia Wengi Wanamuamko Na Facebook,insta,twitter Na Social Net,nitafanya Nusu Saa Sh.300 Tu,pia Gharama Za Bundle Itakuwa Ni Rahisi Na Itanilipa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…