Business ideas (Bure)

Mtu aliyemaliza degree ya ualimu ana qualify kusoma
M. A Business Admnistration ?
 
Safi.
Aise, mimi nimependa idea ya No 3 Car wash.
1. Nafahamu nahitaji kwanza eneo
2. maji (kisima, maji ya bomba) ....... (sijapata bei ya uchimbaji kisima)
3. Vijana wa kuosha magari (hawa watalipwa kulingana na kazi)
4,. .....motor na pump ile wanatumia ku- fasten maji - jina sahihi sijafahamu (sijui bei yake)
5. generator kwa ajili ya umeme (best, cheap and efficient generator sijazifahamu
6. kujenga eneo la kuoshea gari
7. Variable costs (hizi nafikiri si kubwa soap, vitambaa vya kuoshea, ving'arishi.......)

Nimetaja vile ambavyo nimekuwa naviona kwa waoshaji, ndio maana hata majina ni kama nimeyataja bila usahihi sana.

Tafadhali, kama unafahamu vya kutosha biashara hii nimeipenda na ninapenda kuifanya licha ya kuwa sina fedha kwa sasa ila najipanga.






 
Safi Mtanganyika kwa entrepreneurship ideas. Nakushauri ufungue darasa la ujasiriamali
 
Ndugu zanguni nimefarajika kwa elimu yenu juu ya masuala ya biashara,naombeni mnisaidie ninae rafiki yangu ana kiwanda cha kutengeneza mifuko ya magunia ya cotton,kikubwa ama changamoto ni masoko nawaombeni msaada wenu kwa huko.
Ahsanteni
 
Ndugu zanguni nimefarajika kwa elimu yenu juu ya masuala ya biashara,naombeni mnisaidie ninae rafiki yangu ana kiwanda cha kutengeneza mifuko ya magunia ya cotton,kikubwa ama changamoto ni masoko nawaombeni msaada wenu kwa huko.
Ahsanteni

Mkuu jee mmeshafanya mchanganuo (analysis) ya kwamba mmnamlenga nani kwenye masoko? Pili jee mnamchakato gani wa kuyafikia haya malengo? Mnataka kwenda kwa wateja wadogo wadoho moja kwa moja au mnataka kwenda kwenye wasambazaji moja kwa moja.
 
THANKS FOR THE BUSINESS IDEAS THAT YOU SHOWED OR LISTED
STILL SO NOT UNDERSTAND MOBILE ENTERTAINMENT HOW IT WORK.
COULD YOU EXPLAIN ABOUT ON HOW IT WORKS ??
Mkuu hii inabidi uchonge trailer ambalo unaweza kuvuta, kisha ndani weka Big screen mbili TV nununua PS3 au Xbox, weka ndani sound system na viti. Unakuwa una peleka trela kwenye event za watoto kama birthday, wazazi wanakodi for hour. Weekday fanya partnership na shule hizi za St. Fulani na chekechea
 

Upo sawa mkuu, nibora kujipanga kabla huna mtaji kuliko kuwa na mtaji bila kujipanga. Unafanya vyema kabisa mkuu
 
Asalam aleykum naomba nisaidie tuseme una million ishirini unataka kufanya biashara zanzibar to dar au dar to zanzibar utafanya biashara gani na italipa ?
 
Nunua Vifaa Used kutoka Zenj leta Dar

Ni vzr zaid kama utakuwa unachukuwa Tenda mbali mbali za mahitaji ya watu

Zen unazamia Zenj unachukua mahitaji yako

Unawapelekea mahitaji yao

Ila usije Dumbukiza iyo pesa yote kwa Biashara Mdogo mdogo tuu
 
bado na amini kwa biashara ya buubaa, ng'ombe wanaouzwa karagwe bei ya kutupa sbb ya ukame inalipa hela nyingi kwa kipindi kifupi sana ila watz nadhan hatujaona kama ni fursa japo kwa wenzetu wanaKaragwe ni janga.
 
Mubarikiwe wote mnaochangia na kutoa elimu jinsi ya watu wanavyoweza kujikwamua. Ombi langu kwa vijana ni kuwa na idea kwanza kabla hujawa na mtaji na siyo kuwa na mtaji ndiyo utafute idea. Kwani pindi unapokuwa na wazo inakupa muda mzuri wa wewe kulifanyia upembuzi zaidi na kwa undani kuliko kuwa na mtaji kwanza kwani utajikuta unawekeza katika kitu ambacho hujakifanyia upembuzi vizuri
 
Mawazo mazuri sana nimependa namna wachangiaji walivyojitoa. Ila kiukweli mtaji ni changamoto.
 
Delivery

Bado tz tupo nyuma,hasa kwa vya kula, unaweza kuwa na scooter mbili tatu special kwa delivery, kwa wateja wa online pengine spending 30,000 ya cha kula deliver free.

24 hours

Kufanya biashara wakati wowote, hii utapiga bao sana, kwa biashara za usiku.

Usalama

Lazima uwangalie usalama wa biashara yako, hasa nyakati wa usiku, kwa mfano unauza chakula ukifika muda kuazia saa sita ya usiku unafunga na kuwacha window Maalum yakuhumia wateja fast take away food. Badala ya wateja kuingia ndani ya eneo lako, wengine sio wateja.

Kila baada ya muda pesa ku ondoa kwenye biashara yako na kupeleka bank or safe place.

Camera kugunga sehemu za biashara, cctv, hii ni kwa ajili ya kuwatambua wanao ingia na kutoka, ikiwezekana weka chumba Maalum cha cctv, kuwa na mawasiliano ya vituo vya polisi.
 
Nimefaidika na huu uzi, mke wangu amesomea ujasiria mali, hapa nilikuwa na fikiria jinsi ya kumsaidia na zaidi ni kuwa na machine za kutengeza package iwe plastic bag na chupa.

Nipo katika kufanya research ya mashine ninayo hitaji na uwezo wangu, nimefuatilia kwa mfano chupa za kutia shampoo na shower gel mpaka niende Kenya kununua.

Jengine nimefikiria kujenga eneo Maalum la kufanyia kazi. Kwa sasa biashara zetu tunatengeneza nyumbani.

Nime taget kununua, milk cream separate na mashine yatoa maganda ya tomato na kokwa kwa ajili ya kutengeza tomato paste. ..n.k kwa kuanzia.
 
Ivi naombeni ushauri, kw sasa nawez nkanzisha mradi gani ambao utaniletea maendeleo au nifanye biashar gan itakayowez kunpa faida kubwa,?
 
Habari wakuu natumaini mtakuwa poa,

Nataka kuanza kufanya biashara ya nafaka mf. mchele, maharage kunde n.k lakini ni kuchukua mkoani na kuuza Dar kwa reja reja lakini sijui wapi pa kuanzia na mikoa gani naweza kupata kwa bei rahisi na mimi nikapata faida. Nina mtaji wa ml2.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…