Tutor B
JF-Expert Member
- Jun 11, 2011
- 9,025
- 6,598
Business Ideas (Mawazo ya Biashara)
Ikumbukwe kwamba jambo lolote huwa linaanzia kwenye wazo. Hivyo hata biashara yoyote unayoiona inaendelea ilianzia kwenye wazo. Niliwahi kuandika hapa JF kwamba kuna mawazo ya biashara na nikatoa list yake. Waliojitokea kuhitaji mchanganuo wa mawazo hayo wanaendelea vizuri. Nawapongeza; ila napenda kutoa maelezo kwa ufupi kuhusu kile tunachokitoa kwa wahitaji – ni WAZO LA BIASHARA.
Wazo ndo jambo la msingi ili mtu uweze kufanya jambo lolote. Katika mawazo hayo tunatoa maelezo kwa ufupi kwa vipengere vifuatavyo:-
UTANGULIZI (INTRODUCTION)
Haya ni maelezo kwa ufupi kuhusu biashara / huduma husika. Si kwamba kila ninachokijua mimi kila mtu anakijua; na si kwamba unachokijua wewe mimi nakijua. Hivyo maelezo kwa ufupi yatakupa mwanga kuhusu wazo la biashara husika.
KIWANGO CHA UZALISHAJI
Haya ni makisio ya uzalishaji ndani ya kipindi maalum (siku / mwezi / mwaka n.k)
NJIA ZA UZALISHAJI
Haya ni maelezo kwa ufupi kuhusu njia zinazotumika kwa ajili ya kuzalisha bidhaa husika. Hapa ndipo panahitaji maarifa kwa ajili ya kazi husika. Maarifa yanapatikana kwenye vyuo / vituo vya mafunzo ya ujasiriamali. Pia unaweza kutangaza nafasi ya kazi kwa wale wenye maarifa hayo. Inakuwa vyema wewe mwenye biashara kujua walau mambo ya msingi kwenye shughuli unayotaka kuanzisha.
MALIGHAFI
Hizi ni malighafi / vitu vinavyohitajika kwa ajili ya kuzalisha bidhaa husika. Mfano nitakapokufundisha namna ya kutengeneza chips – malighafi ni viazi mbatata, mafuta na mayai.
VITENDEA KAZI
Hivi ni vifaa kwa ajili ya kurahisisha utendaji kazi wako ili uweze kufikia uzalishaji uliotazamia.
KIPIMO CHA UWEKEZAJI
Haya ni makisio ya mtaji pesa unaohitajika kwa ajili ya shughuli husika. Hapa utaelekezwa gharama za vifaa vya kuanzia, gharama za kuendesha, na kile kitakachopatikana.
UCHAMBUZI WA SOKO
Haya ni maelezo kwa ufupi kuhusu wahitaji wa mali / bidhaa utakayoizalisha. Zipo bidhaa ambazo watumiaji wake wa ndani ni wengi kiasi kwamba huhitaji kuangaika kupeleka nje ya nchi; na pia zipo bidhaa ambazo uhitaji wa ndani ni mdogo lakini nje zinahitajika sana. Hivyo katika kipengere hiki utajuzwa ni wapi pa kuuza bidhaa yako.
GHARAMA ZA MRADI
Huu ni mkusanyiko wa majedwali yanayoonesha yafuatayo:-
1. Mtaji wa kuwekeza
2. Gharama za uendeshaji
3. Gharama za mradi na makisio ya mauzo
4. Uchambuzi wa makisio ya faida tarajiwa.
UPATIKANAJI WA MALIGHAFI NA VIFAA KAZI
Katika kipengere hiki tunasisitiza zaidi mbinu za kupata malighafi na vifaa kazi. Siku hizi dunia ni kama kijiji; hivyo unaweza kununua chochope – popote pale na ukafikishiwa ulipo pasipo wewe kusafiri. Hapa ndo elimu ya matumizi ya computer inapoonekana umuhimu wake.
UWEZESHWAJI WA SERIKALI
Kwa kuwa mawazo mengi yanahusika na uzalishaji wa bidhaa, ni ukweli usiopingika kwamba serikali ya awamu ya tano (Tanzania) imeweka wazi kuhusu namna ya kuwasaidia wajasiriamali wa wadogo na wa kati kuanzisha miradi ya uzalishaji. Katika hili hatuliongelei sana kwa sababu kila mtu popote alipo anajua wazi kwamba kuna msukumo mkubwa sana wa kuifanya Tanzania kuwa ya viwanda.
Baada ya kupata mawazo haya wewe kama mjasiriamali unapaswa kufanya yafuatayo:-
BAADHI YA VIPENGERE UTAKAVYOHITAJI KUKAMILISHA NI KAMA IFUATAVYO:
Naenda lunch … nikirudi tutaendelea kulingana na muitikio wa wasomaji.

- Fanya utafiti wa kina kwa sehemu unapotaka kuanzisha mradi wako.
- Angalia mambo yote unayoweza kuyafanyia kazi
- Fuatilia vibari kwenye mamlaka husika
- Chagua sehemu sahihi ya kuweka mradi wako
- Wasiliana na wataalamu wanaohusika na bidhaa husika
- Chagua kwa usahihi ni bidhaa ipi unataka kuzalisha
- Anza kutengeneza mpango wa soko.