Kwanza kabisa lazima uangalie nini unapenda kwasababu kufanya biashara si eti kwamba una "plug 'n play" na vitu vinajipa ni lazima upende kile unachofanya ninavyosema kupenda ni kama vile kuwa kwenye ndoa. Huwezi kesho kusema tuu, 'aah mi pesa zikiingia mambo shega" halafu ukajiachia vipi kama mambo hayata kuwa mazuri?
Kwahiyo jiulize kama wewe unapenda nini, je unapenda kilimo (biashara ya vyakula), wanyama (biashara ya ufugaji), kufundisha (speaker - seminar business), tekinolojia (biashara ya mtandao) n.k. Ondoa hiyo kitu unayosema "biashara gani inalipa". Ukimuuliza Mexence Melo nauhakika atakwambia anapenda mambo ya computer security, information technology n.k
Biashara yoyote inalipa unachotakiwa kufanya ni kuangalia "need" kwa mfano unaweza kufanya ka-survey hata hapa JF kuangalia watu wanamatatizo gani. Kwa kuangalia tuu maswali yanayoulizwa hapa utaweza kuona watu wanashida gani. Sasa kama wewe mjasirimali wa kweli unajiuliza, "hivi nitawasaidiaje hawa watu? Ukipata jibu unatengeneza kamfumo ka kuwasaidia kwa gharama nafuu. Ndiyo biashara ya wenye akili inavyoanzishwa ndugu.
Pia usipende mambo ya mkumbo kwa kufanya kitu eti kwasababu fulani anafanya, wewe kama ni mjasirimali jaribu kusaidia matatizo ya watu na hapo utaweza kupata business idea nyingi tuu. Ukiniuliza mimi kuhusu idea sana sana nitakwambia "internet business" kwasababu napenda "technology" na kitu chochote kinachohusu computer (programming/engineering) au computer science. Sasa kama nikikuambia unaweza tengeneza mahela kwa kutengeneza "cloaking script" wakati wewe haya mambo yanakuboa utaweza vipi kuamini idea yangu ni nzuri?
Kwakuhitimisha tuu jaribu kuangalia hapa hapa Jamiiforums mambo yanayowakera watu halafu jaribu kuyatatua.