Business partner: Mimi ni mhangaikaji na fursa zipo lakini sina mtaji wa kutosheleza

antanarivo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2018
Posts
450
Reaction score
883
Wakuu habari!

Natumaini ni wazima na wale ambao wanapitia changamoto mbalimbali za kiafya Mungu awasaidie ili muweze kurejea katika Hali yenu ya kawaida !

Niende moja kwa moja kwenye point yangu iliyonifanya nianzishe huu Uzi.

Mimi ni mhangaikaji Sana Tena Sana na ninatumia uwezo wangu wote kuhakikisha angalau maisha yangu yanakuwa stable na hii inatokana na mfumo wa maisha yangu toka ninakua Hadi Sasa yaani kwa wale wanaoyajua maisha ya kutokuwa na wazazi wao na hawawafahamu kabisa wanaweza kuwa mashahidi ni namna gani tunahangaika huku na huku ili kupata mkate wa kila siku , tunapitia mengi kwakweli lakini Mungu wetu hajawahi kututupa na hutulinda kwa njia mbalimbali ndo maana bado tuna survive

Binafsi huwa na tabia ya kujifunza vitu tofauti tofauti ili mradi nimeona fursa katika hiko kitu, mpaka Sasa Nina uwezo wa kupata at least sh 12000 Hadi 20000 kwa siku kupitia vyanzo mbalimbali hivyo kunihakikishia maisha ya hapa mjini Kama kula ,pango kusaidia ndugu n.k

Lakini Kuna fursa ambayo ninataka kuifanya tangu muda mrefu na Ina zero risk na faida yake inaweza range Kati ya 10000-50000+ kwa siku moja na hii ni uhakika asilimia 100% lakini changamoto kubwa ni mtaji wa pamoja maana nimejitahidi kutunza kidogo nachopata ili kuanza imeshindikana yaani kutokana na kuwa kipato nakipata daily na nategemea kula hapohapo, pango hapo hapo na ndugu pia hapohapo ko najikuta sifikii lengo na siku zinazidi kusonga

Ombi langu: hii biashara inahitaji mtaji Kati ya 2m hadi 7m haizidi hapo na mtaji huu utaweza kuleta faida ya sh 10000-50000 per day au zaidi itategemea, na kumbuka mtaji hauathiriwi hata Senti 10 na muda wowote unaweza kughairi na hela yako itabaki salama hivyo Kama Kuna mtu ana kiasi hiki na anataka tuingie ubia nipo tayari kumfuata popote nikiwa na full documents zangu zote na hio hela ya mtaji yeye ndo ataicontrol muda wote yaani mnafanya kazi then jioni mnapigiana mahesabu na kugawana asilimia ya faida itakayopatikana na nipo tayari kufanya kazi under his/her control ili iwe rahisi kwake na awe na uhakika kuhusu usalama wa hela yake

Kwa mtu mwenye uwezo wa hiko kiasi anaweza Nipa namba yake inbox au anaweza kunipm ili tuweze kuonana tukayazungumza ana kwa ana

Ahsante
 
Siku hizi kila mtu hutafuta mnyonge wake wa kumpiga
Usiseme hivo mkuu baraka za mtu zipo kwa watu ukiongelea au kukatisha tamaa wengine sio vizuri huwezi jua kwanini mtu mpaka kaamua kuleta andiko Kama Hilo , tungelikuwa na dhamana za viwanja na nyumba Kama wengine tungeenda bank kupata mikopo hakuna mtu anayependa kuomba mtaji kwa mtu binafsi
 
Kama huna cha kucomment kaa kimya mkuu, we umejuaje kama mleta mada ni tapeli[emoji35][emoji35]. Unanyima fursa watu asee.
Ni kweli aisee mtu Kama alikuwa na Nia ya kukusaidia anaacha , hii mitandao sio uadui tujifunze kutoa kauli nzuri licha ya kuwa hatufahamiani
 
Wakuu habari!

Natumaini ni wazima na wale ambao wanapitia changamoto mbalimbali za kiafya Mungu awasaidie ili muweze kurejea katika Hali yenu ya kawaida !
Bro usitake kung'ata pakubwa kama huna kinywa kikubwa. Ng'ata kulingana na ukubwa wa kinywa chako. Nenda taratibu utafanikiwa.
 
usipoelezea hyo ishu hapa huu uzi ni batili na utakuwa na viasharia vya kitapeli

Samahani kwa hayo maneno ila kuaminiana kwa watu wa Sasa hv ni swala gumu sana

Sent from my Infinix X609 using JamiiForums mobile app
 
Ni hatari kwa vijana kukatishana tamaa sisi kwa sisi
Sidhani kama ni kukatishana tamaa, tusiwe overambitious wakati hata madogo bado hatujafanya. Tufanye madogo kwanza, hayo makubwa yatafikia level yetu kesho.
 
Wazo zuri but ukisema zero risk unapotosha mkuu coz kimsingi palipo na zero risk hakuna opportunities

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi pia nna kampuni natafuta partner mwenye knowledges na mtaji watu pesa sio kihivyo kama uko interested njoo pm

Sent using Jamii Forums mobile app
Kampuni si karatasi tu? Pesa ndio kila kitu. Mwenye pesa kuanzisha kampuni anatumia week 2 tu. Una kitu gani cha ziada cha kumfanya mtu aje awekeze kwako? Utaalamu, market share, jina kubwa, ubunifu au nini hasa?
 
Kampuni si karatasi tu? Pesa ndio kila kitu. Mwenye pesa kuanzisha kampuni anatumia week 2 tu. Una kitu gani cha ziada cha kumfanya mtu aje awekeze kwako? Utaalamu, market share, jina kubwa, ubunifu au nini hasa?
Ofcourse pesa imeshawekezwa na kama unavyojua watu wanaweka pesa ili izae pesa kuhusu ufafanuzi ni kwamba watu wengi wanasahau kuwekeza kwenye maarifa ndo maana nikasema natafuta mtu ambaye ata add kitu kwenye kampuni yangu what i mean ni mtu ambaye ana mtaji wa watu na awe na potentials kwenye ishu ambazo kampuni yangu inahusika nayo not everybody can join my team

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu heb jarib kuni pm then unipe japo introduction kdogo...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…