Business partners for Black soldiers fly production

Joined
Dec 24, 2019
Posts
12
Reaction score
2
Nategemea na nipo kwenye process ya kuzalisha Black soldiers fly ambao watatumika kama chakula cha mifugo ikiwemo kuku, nguruwe, samaki na vinginevyo.

Pia mabaki yake yanayopatikana yatatumika kama mbolea. Hivyo ninahitaji watu walio serious nitakaoshirikiana nao katika katika kufanikisha hili.
 
Mradi wote unagharama ya kiasi gani, na uwekezaji utakuwa mkoa gani?
 
Samahani kwa kutoorodhesha hili.
Mradi utakuwa Dar es Salaam. Kwa kuanza itabidi tuingie gharama ya vifaa vya uzalishaji ambavyo havitagharimu milioni 5.
 
Toa elimu kidogo kuhusu huu mradi. Black soldiers fly ni nini, malighafi, mchakato wa uzalishaji, soko n.k. Nina imani wengi hatuujui huu mradi. Natanguliza shukrani mkuu.
 
location ya mradi mkuu na vyanzo gani utatumia? upatikanaji wake ukoje na gharama za usafiri. pia nategemea umewahi kufanya small scale ukawa na uzoefu nao.
 



je hapo unamaanisha pia utashirikiana na mwekezaji pia kwenye kilimo?
 
Black Soldier fly Larvae Productions inahitaji mtaji mkuu, million 5 ni ndogo sana,

Naifanya Arusha naijua fika, pia ni labaour intensive.

Na unapaswa juwa na eneo lako nje ya makazi ya watu kwa sababu we fly wanao kuwa kwenye nyumba yao ikitokea ajari wakachotoka basi ni balaa tupu mtaani lazima wakazi waandamane mbaya na unaweza pata misuko suko ya kufa mtu.

Kule Mkuranga kuna Wazungu iliwatokea ilikuwa Balaa tupu.
 
Samahani kwa kutoorodhesha hili.
Mradi utakuwa Dar es Salaam. Kwa kuanza itabidi tuingie gharama ya vifaa vya uzalishaji ambavyo havitagharimu milioni 5.
Million 5 haitoshi, vifaa vya kuanza navyo na bado means ya ku collect waste za kuwalisha, labda uwe na Gari pick up yako.
 
Black Soldier Fly Larvae au BSFL ni protein itokanayo na hao Black soldier fly.

Kwa tunako elekea itakuwa na soko sana make Soya ambayo ndo chaanzo kikubwa cha protein kwa sasa upatikanaje wakw ni shida.

Vitu kama mabaki ya samaki nayo ni shida kwa sababu ya competition kati ya Binadamu na Mifugo, na hapo Binadamu ndo anaye wini.

So BSFL ni wazuri sana na ndiko Dunia inako elekea.
 
Nimesema m5 kwa sababu kuna vitu tayari ninavyo. Naishi DSM ila mradi utafanyika yombo mpera.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…