Business Planning as the thinking Process

Masokotz

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2018
Posts
3,713
Reaction score
6,121
Moja kati ya changamoto ambazo huwa nakutana nazo mara kwa mara ninapokuwa nafanya kazi na wateja wangu ni tatizo katika uandaaji wa Business Plan.Kwanza kabisa wengi hushindwa kutofautisha kati ya Business Plan Template na actual business plan.Wote tunajua na kuamini kwamba Failure to Plan is Planning to failure.Kauli hii ina ukweli mkubwa sana kwani asilimia kubwa ya watu waliofeli katika Biashara na mambo mengine ni wale walioshindwa Kufanya Proper Planning.

Business Planning sio aina ya uandishi bali ni aina au mfumo wa kufikiria.Unapokuwa ni mjasiriamli mdogo,mkubwa au wakati unahitaji kuwa na Business Plan ambayo itakuongoza katika biashara yako.Hii itakuwa ni ramani yako na muongozo wako wa kuanzisha na kuendesha Biashara yako

Business Plan ni mfumo wa kufikiri wa Mjasiriamali yeyote yule.Kama mfumo wako wa Kufikiri haujajengeka kufikiri kama mjasiriamali basi tambua kwamba kuna tatizo kubwa katika kukua kwa biashara yako ambalo ni wewe.

Je unajengaje huu mfumo wa kufkiri kijasiriamali?
Kwanza lazima utambua hitaji lako kuu ni nini.Pili ni lazima utenge muda maalum na ratba maalum kwa ajili ya kufikiri kuhusu biashara yako.Tafuta taarifa zote muhimu kuhusu seta yako ndani na nje ya nchi na uhakikishe kwamba unajenga tabia ya kuona fursa ndani ya changamoto.
Nakutakia kila la heri katika safari yako ya ujasiriamali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…