Butiama pataendelea kuwa mahali muhimu.

Joyce SARINGO

New Member
Joined
Mar 12, 2015
Posts
3
Reaction score
0
Kutokana na historia inaonekana kwamba kabila la wazanaki lina zingatia na kuenzi MAADILI NA TUNU za utu, upendo, Uwajibikaji, uzalendo, Amani na Utulivu ambayo wamekuwa wakiirithisha kizazi hadi kizazi.

Kila Kiongozi aliyepata fursa ya kupata baraka toka kwa wazee wa kizanaki wamekuwa viongozi bora na wazalendo wa kweli wenye uchungu na Taifa hili.

Nyerere Alipata bahati ya kuwa mwanafamilia wa wazanaki ambae aliongoza Taifa kwa Ufanisi mkubwa akilitoa katika makucha ya wakoloni, na baadae Mkapa alipata baraka hizo, pale Butiama, kila mtu ni shahidi juu ya mafanikio yake katika uongozi wake uliotukuka. JE Ni kiongozi yupi atakaebahatika kupata baraka hii?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…