Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 276
- 473
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Mwalimu Julius Nyerere, Joseph Butiku amesema siku hizi siasa zitaka kugeuzwa kama mchezo wa kihuni huku akidai kuwa nchini kuna Watu wanaopenda siasa za kihuni.
Akizungumza September 10, 2024 amesema kuwa jamii haitakiwi kuunga mkono wanaohitaji uongozi kwa kutumia njia za 'kihuni' ikiwemo kutekeleza mauaji au kutoa rushwa.
"Taifa letu halijafundishwa siasa za kihuni hata siku moja, tulipata kiongozi Baba wa Taifa (Mwl. Nyerere) alitulea vizuri hakuwa muhuni na kama tunamuita Baba wa Taifa basi sisi Watoto wake hatutarajii kuwa wahuni wa kuua Watu."anasema Butiku
Ameongeza"Kwahiyo siasa siku hizi inaanza kugeuzwa kana kwamba ni mchezo wa wahuni, SIVYO . Napenda Watanzania wasikubali kwamba wana siasa ya kihuni HAPANA"
Aidha anadai "Ndani ya Nchi yetu wapo watu wanaopenda siasa ya kihuni, lakini mfumo wetu ni wa siasa ya kiungwana."
"Hutafuti cheo kwa kuua wenzako ukifanya hivyo wewe ni muhuni, lakini zaidi hutafuti cheo kwa kuhonga, kununua haki ya wapiga kura na vilevile wewe raia husitake hela za wanaotafuta vyeo, raia wetu nao wanapokea hela pamoja na baadhi ya maaskari."
Amesisitiza kwamba unahitajika uwajibikaji kwa kuheshimu Watu ikiwemo kulinda maisha yao na mali zao, lakini amesema kuwa kwa sasa Watu wameanza kuingiwa na uoga, amedai kuwa wapo wanaojua ukweli wa mambo mbalimbali lakini hawasemi kwa kuhofia kutendewa visivyo.
"Katika kuwajibika inahitaji ujasiri wa moyo unaotoka na imani , kwamba watu ni watu wanastahili kuheshimiwa na maisha yao yanastahili kulindwa na mali zao, katika hilo hakuna uoga Taifa hili limeanza kuwa na Watu waoga.
Anaongeza" Mjue Demokrasia hupewi kwenye sahani inatakiwa huipiganie. Tanzania tumejengewa msingi mzuri sana tukibabaika na uoga na unafiki hatuwezi kufika." Amesema Butiku
Pia, soma: Joseph Butiku: Vyombo vya ulinzi na usalama visijifanye havijui mambo yanayoendelea nchini