Butiku:- Si Dhambi Kuipigia Kura ya HAPANA Katiba Pendekezwa

Butiku:- Si Dhambi Kuipigia Kura ya HAPANA Katiba Pendekezwa

Dupe

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2013
Posts
1,668
Reaction score
811
Mbeya. Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku amesema si dhambi kwa wananchi kupiga kura ya hapana Katiba Inayopendekezwa.

Akizungumza juzi jioni kwenye mdahalo wa Katiba ulioandaliwa na taasisi hiyo ambao ulifanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (Teku) jijini Mbeya, Butiku alisema kura ya Hapana au Ndiyo, zote zinatoa fursa sawa kwa wananchi kuamua kwa utashi wao.

Katika mkutano huo uliohudhuriwa na mamia ya wakazi wa Mbeya, Butiku aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba, alieleza kuwashangaa viongozi wa vyama na Serikali kuwachagulia wananchi kura ya Ndiyo.

Akitolea mfano wa chama chake cha CCM, Butiku alisema hakitakiwi kuwahadaa Watanzania na kuwataka kuipigia kura ya Ndiyo katiba hiyo, badala yake kiwaache waamue wenyewe.

Aliwataka wananchi watumie muda huu kuitafuta nakala ya Katiba Inayopendekezwa, waisome na kuielewa ili hatimaye waamue ama kuipigia kura ya Hapana au Ndiyo.

“Mchakato huu una mambo makuu mawili ya kuamua ambayo ni kura ya Ndiyo au Hapana. Hivyo basi kupiga kura ya Hapana siyo dhambi kwani inatoa nafasi kwetu sote kukaa tena na kuangalia upungufu uliojitokeza na kilichosababisha upungufu huo nini ili tusirudie tena makosa,” alisema Butiku na kuongeza:

“Kura ya ndiyo inamaanisha tunaikubali Katiba Inayopendekezwa, hata ikiwa haina mashiko itaendelea kutumika kwa vile mmeikubali, lakini nisisitize kwamba kura ya hapana siyo dhambi, ipo kisheria na asije mtu akawaambia mpigie kura ya ndiyo.

Alisema kabla ya kuipitisha au kuikataa Katiba Inayopendekezwa ni vyema ikashindaniwa kwa hoja na si kwa nguvu au ngumi huku akiwataka vijana nchini kutothubutu kujiingiza kwenye mikumbo inayoweza kusababisha nchi ikaingia kwenye machafuko.

Profesa Baregu

Akizungumza katika mkutano huo, Profesa Mwesiga Baregu ambaye pia alikuwa mjumbe wa tume hiyo, alisema licha ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kuahirisha Kura ya Maoni ya Katiba Inayopendelezwa kwa muda usiojulikana, kwa mtazamo wake anaona haitakuwapo kabisa.

“Mimi Baregu, nasema hivi siyo kwamba imeahirishwa, nafikiri haitakuwapo kabisa kura hiyo na hii inatokana na ambavyo mchakato mzima ulivyoendeshwa na si kwa maudhui yaliyomo kwenye Katiba Inayopendekezwa, bali ni kwa namna ambavyo Bunge Maalumu la Katiba lilivyofanya na uandishi wake.”

Alisema katu Watanzania wasije wakawa na papara na Katiba hiyo hata baada ya Uchaguzi Mkuu, bali wawe na subira kwani wakiiendea haraka inaweza ikaipeleka nchi mahala pabaya na kujikuta ikitumbukia kwenye machafuko yasiyo na tija.

Hamphrey Polepole

Mjumbe mwingine wa tume hiyo, Hamphrey Polepole alisema Watanzania wanatakiwa kutambua kwamba Katiba siyo kitu cha kuamuliwa na wanasiasa au kuamua kwa kusikia tu, bali ni kwa kushiriki katika kuipigia kura ya hapana au ndiyo kwa kutumia utashi wao binafsi.

“Katiba hii siyo ya wanasiasa ni ya wananchi wenyewe, lakini cha kushangaza hapa ni wanasiasa wanavyochukua nafasi kubwa ya kuuteka mchakato huu na hii yote wanataka wapate nafasi ya kulinda masilahi yao na kuendelea kututawala watakavyo, hivyo ndugu zangu wa Mbeya na Watanzania wote chukueni hatua.”

Alisema anawashangaa hata viongozi wakubwa ndani ya vyama na Serikali kuendelea kuipigia ‘debe’ Katiba Inayopendekezwa kwa kuwahadaa wananchi kupiga kura ya ndiyo wakati wakitambua fika kwamba haijakidhi matakwa Watanzania.

Mjumbe mwingine wa iliyokuwa Tume hiyo, Ally Saleh alizungumzia masuala ya muundo wa Serikali, alishangiliwa na mamia ya watu waliofurika ukumbini hapo aliposema: “Mwenyekiti wangu hapa (Butiku) kasema kwamba kura ya hapana siyo dhambi, lakini mimi nasema hivi, watu wasipige kabisa kura.”

Chanzo:- Mwananchi
 
Wananchi tujitokeze kwa wingi kujiandikisha wakati utakapofika kwa ajili ya kupiga kura ya maoni kuhusu katiba inayopendekezwa,katiba ni ya watanzania wote,kura ya ndio kwa katiba inayopendekezwa ni muhimu ili taifa lisonge mbele,tuachane na propaganda na siasa zaupotoshaji,tanzania kwanza
 
Hima hima Watanzania wakati ndiyo huu, wakati unaokubalika ndiyo sasa. Ukitangaziwa tuu! kujiandikisha kaza buti ewe mama, baba, kaka, dada, mjomba, shangazi, jirani na Mtanzania yeyote mwenye umri wa kuanzia miaka 18........, changamka uwe tayari simama timiza wajibu na haki yako ya Kikatiba.
 
Kuna nanihii fulani jana walikuja na upuuzi wao hapa kuwa Pole pole kaikubali hii Katiba, pumbafu kabisa ningekuwa Invisible ningewaondoa kabisa duniani
 
Kuna nanihii fulani jana walikuja na upuuzi wao hapa kuwa Pole pole kaikubali hii Katiba, pumbafu kabisa ningekuwa Invisible ningewaondoa kabisa duniani

Jiondoe mwenyewe kwanza!!!afu uwaondoe wenzako!!!
 
Hahahahagahahaaaaaaa

Haaa au sio mimi hivi si ndo wewe ulikuja na unabii wako wa uongo kushawishi wana JF kuhusu anguko la Tz kwa sababu ya Sitta na ukawa unashabikia ukiwa mtumishi mwaminifu wa Mungu, ghafla ukabadilika ukaanza kutukana mitusi ha ha ha ha ha mpaka leo unatukana huna tofauti na Wagalatia walioanza kwa Roho wakamaliza kwa mwili mchumia tumbo wewe na umetumwa wewe unabii wako wa uongo!!!tokaaa
 
Hahahahhahahaahahaaaaaa too low for you! Nishawishi JF mimi? hahahahhahaaahaaaaaa
Haaa au sio mimi hivi si ndo wewe ulikuja na unabii wako wa uongo kushawishi wana JF kuhusu anguko la Tz kwa sababu ya Sitta na ukawa unashabikia ukiwa mtumishi mwaminifu wa Mungu, ghafla ukabadilika ukaanza kutukana mitusi ha ha ha ha ha mpaka leo unatukana huna tofauti na Wagalatia walioanza kwa Roho wakamaliza kwa mwili mchumia tumbo wewe na umetumwa wewe unabii wako wa uongo!!!tokaaa
 
Butiku anajitambua na anafanya lililo sahihi kwa mustakbali wa wajukuu na vitukuu wake
 
Piga kura ya ndio kwa katiba inayopendekezwa wakati utakapofika,jiandikishe ili utimize haki hii ya msingi
 
The joining date haikuhusu, we alokwambia kusoma kufika PHD ndo kujua mambo nani! Kutangulia sio kufika, tarehe ya kujiunga haihusiani na kujua au kutojua kujibu hoja, suala hapo ni kwamba umeishiwa hoja, kapumzike hapa hupawezi.
hahahahhaaaaa ni shida sana unapo-argue na mtu mwenye mihemko kama wewe! nadhani better niku-ignore tu!
 
Jitokeze kujiandikisha wakati utakapofika ili mwisho upige kura ya ndio kwa katiba inayopendekezwa
 
Hima hima Watanzania wakati ndiyo huu, wakati unaokubalika ndiyo sasa. Ukitangaziwa tuu! kujiandikisha kaza buti ewe mama, baba, kaka, dada, mjomba, shangazi, jirani na Mtanzania yeyote mwenye umri wa kuanzia miaka 18........, changamka uwe tayari simama timiza wajibu na haki yako ya Kikatiba.

tunatimiza wajibu wetu kwa kuhamasisha na kupiga kura ya HAPANA kwa katiba ya Chenge.
 
makanisani waraka wa kuipigia katiba kura ya hapanaa unasambazwa.nikimwana ccm mwanifu nasema KATIBA MPYA.haipo kwenye ilani ya CCM.ilani inasema tutaanzisha mahakama ya kadhii
 
Back
Top Bottom