member: 188652"]
Hapa nitakupa ABCDs za huko japo nimetoka kitambo. Kufika kijiji cha buzi ni rahisi sana, na ukifika kijijini hapo kwanza tafuta kufahamika kwa mtendaji wa kijiji atakayekutambulisha kwa wenyeviti wa vitongoji na kijiji (nasema mtendaji kwanza kwasababu ndiye rahisi kujua ofisi yake kabla ya kujua za wenyeviti na ofisi yake ipo karibu za Buzi Dispensary).
Ukifika bukoba mjini uliza zinapopaki daladala za bugabo (ni mita chache kutoka stendi kuu), hapo pia kuna taxi.
Ukipanda taxi unamwambia akupeleke buzi (nauli ilikuwa kuanzia 30,000 kutegemea na kitongoji unapoenda maana kijiji ni kikubwa na ukimwambia dereva adhima yako anakupa bei kulingana na mizunguko), ukipanda daladala za kwenda bugabo unashuka kituo kinaitwa Kibengwe na ni kacenter kadogo kiasi ila kamechangamka ni kama km 10 au 12 toka mjini na nauli ilikuwa 1,000 hadi 1,500), hapo kuna vijana wa bodaboda wa kutoka maeneo mbalimbali lakini ukimpata wa kutoka kijiji hicho ni rahisi maana wanakijua kijiji kizima kuliko wasio wa kule ingawa wote wanakupeleka bila shida. Nauli ilikuwa kuanzia 2000 na kuendelea kutegemea na unapoenda. Umbali wa kutoka hapo kibengwe ni kama km 6 au 7 kufika kijijini buzi baada ya kuvuka kijiji cha kayugwe.
Kijiji kipo ktk kata ya kaagya na kina vitongoji vinne (kabera, buguruka, miziru na kishura na kuna kipindi walikuwa wanataka kiwe kata) Ni kijiji chenye shule 2 za msingi (Kashanje primary na Buzi Primary na zilikuwa vizuri kimiundombinu na taaluma), Pia Zahanati moja ya kijiji cha Buzi ipo karibu na Kashanje primary na nilioneshwa msingi wa madarasa kwa ajili ya shule ya Sekondari ingawa niliambiwa ulisimama tangu miaka ya 2000 huko. Ni kijiji chenye kanisa 1 la KKKT (hili kanisa lipo karibu na shule ya msingi Buzi) pia yapo makanisa mawili madogo ya Romani na makanisa mengine ya madhehebu ya orthodox, n.k,..
Niliambiwa ni kijiji kilichotangulia kuwa na wasomi wengi ktk tarafa ya bugabo ingawa wengi wanakaa mikoani. Kuna Prof kama siyo Dr niliambiwa yupo SUA anaitwa Ndyetabulla anaweza akakupa taarifa kadhaa japo sikumtafuta kutokana na muda. Niliambiwa kijiji kina mapadri kadhaa na watu wengi ni wakristo wa rc na kkkt, waislam ni wachache mno.
Kiujumla ni kijiji chenye mandhari nzuri kikizungukwa na miti ya kupandwa na ya asili (watu wanapanda miti sana) na wanakarimu wageni (kwa uzoefu wangu). Watu wake wanalima Kahawa, Migomba, mihogo, viazi vikuu na vitamu, mahidi kidogo, maharage, na njugu mawe, wafugaji wa ng'ombe na nguruwe ni wachache ila wafugaji wa mbuzi, kuku na bata ni wengi. Pia kulikuwepo na wafugaji wa samaki kwenye mabwawa maeneo wanaita kango (kama sijakosea).
Vijana wengi hawapendi sana kazi za shamba na wanatoka kutafuta mikoani. Barabara zinapitika muda wote ila umeme ulikuwa haujafika na kwa vijiji jirani wachache wanatumia solar. Miundombinu ya maji haiko vizuri japo wana vyanzo vingi vya maji. Mawasiliano ya simu yapo vizuri. Na huduma za maduka ya bidhaa yapo.
Kimakazi wako vizuri na wanajitahidi kujenga kutegemea na uwezo wa mtu. Kwenye kuoa au kuolewa hakuna tofauti na pengine ni wewe tu na ulipompata mwenza. Binti wa buzi wanaolewa buzi na maeneo mengine na vijana wanaoa buzi na maeneo mengine. Zahanati yao inapokea na watu kutoka wilaya ya Misenyi.
Kuhusu kula watu sikutoka na jibu sahihi ingawa niliamini ni story za kusadikika maana wazee walinipa taarifa tofauti na vijana walivyokuwa wananiambia. Wazee wanasema hakuna mtu aliyewahi kuliwa bali zilitungwa hadithi za kusadikika kutokana na ugomvi wa familia moja (hapa kuna taarifa ndefu sana ukifika na ukakaa na wazee watakwambia).
Vijana na watu wa vijiji jirani wana kauli ya NILISIKIA na mdo nilchotoka nacho na mpaka vizazi vinavyokuja vinaambiwa hivyo na inabaki kauli ya nilisikia ingawa wapo waliokuwa wanasema wameoza binti zao huko na wengine vijana wao wameoa huko.
Kiujumla sikuona tofauti yoyote ya kiimani iliyopishana na maeneo mengine ambayo nimebahatika kukaa.