Bwana mdogo ashinda kesi ya mtoto mahakamani!!!

Bwana mdogo ashinda kesi ya mtoto mahakamani!!!

Upanga

Senior Member
Joined
Jun 18, 2007
Posts
145
Reaction score
50
Bwana Mdogo ameshinda kesi Mahakamani ya kutaka kukaa na mtoto wake wa miaka tisa baada ya mzozo na mama mtoto wa karibu miaka kadhaa!!
Bwana Mdogo alipeleka malalamiko yake serikali za mitaa kudai kukaa na mtoto baada ya kuona mama mtoto hamjali wala hampi matunzo mazuri mtoto,lakini huyu dada alikataa katakata kukubaliana na Serikali ya mtaa na hivyo baba mtoto kuruhiswa kwenda ustawi ili wakawekewe mambo sawa!
Hata hivyo kule ustawi mama mtoto akashindwa tena lakini akagoma kumruhusu mtoto aende kwa baba.Ustawi wakampa ruhusa baba aende mahakami.
Jana kesi imeisha baada ya kusikilizwa almost miezi minne,na mahakama imeamuru baba apewe mtoto,lakini mama amekataa kutoa mtoto kwa kigezo cha kusema anakataa rufaaa!
Je rufaa ambayo mtu anafikiria kukata inaweza zuia adhabu isitekelezwe?
Tunaomba michango yenu kwa hili.
 
Nashauri ungepeleka jukwaa la sheria, humu kwenye siasa sidhani kama ni mahala pake.
 
Inawezekana nimekosea nini!, hivi nipo ukurasa wa siasa au?!! Ngoja niangalie.....
 
Hii inaashiria jf sasa haina utaratibu ama? Mbona kama sielewi elewi?
 
maamuzi ya mahakama lazima yatekelezeke ili hali rufani ikiwa inasubiri kama nimekuelewa sawa sawa ni kwamba mama wa mtoto ameweka nia ya kukata rufaa ila bado hajakata ....... kama ndio basi inabidi atekeleze icho kilicho amuliwa na mahakama kwanza kinga anayoweza kupata kwa sasa ni kukata hiyo rufaa mara moja kisha kupeleka nakala ya iyo appeal application kwenye hiyo mahakama iliyo toa iyo hukumu ili maamuzi yake ya baki kuwa steady while waiting for the appeal decision away 4m that ampatie 2 huyu baba mwanae yasije yakamkuta mengine bure as kukaidi amri ya mahakama nalo ni kosa lenye adhabu kisheria
 
Thanks tumejaribu kwenda kuchukua mtoto lakini mama amekataa na kuepusha vurugu tulienda omba msaada wa polisi
lakini polisi vituo viwili tofauti wamekataa kwa kusema kuwa,kwa vile ni hukumu ya mahakama basi kesi ya madai huwa lazima isubiri siku 30 za rufaaa,kama haijakatwa mahakama kupitia hakimu huwa anatoa amri kwa mama kukabidhi mtoto
kinyume cha hapo ni kuvunja sheria.
Hatuna cha kufanya maana sheria zina upana wake,tunaomba ushauri kama upo.
 
Ondoa dhana hiyo ndugu yangu siyo kila mtu ni mwana siasa tunaomba tueleweshane tu mambo ya sheria yanavyokwenda
sisi tupo Dar!eneo la Magomeni hatuna ndugu yeyote katika siasa.
 
Back
Top Bottom