Bwana na Bibi Harusi wajinyonga

Bwana na Bibi Harusi wajinyonga

Wakulonga

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2012
Posts
762
Reaction score
771
Katika hali ya kusikitisha nchini kenya bwana na bibi harusi wameamua kujinyonga ili kuepukana na madeni baada ya harusi yao.
=======
Mtandao wa Kenya today umeripoti kuwa wanandoa wawili Keneth na Mary Odipo waliofunga ndoa ya kifahari huko Kisumu wiki mbili zilizopita wamejiua kutokana na kuandamwa na mzigo mkubwa wa madeni.

Inaelezwa kuwa ndoa yao iligharimu kiasi cha Ksh 7.9Million, sawa na karibu Milioni 170 za Kitanzania, sehemu kubwa ya fedha hizo zikiwa ni mkopo.

Keneth alikusudia kufunga ndoa ya Ksh 500,000 sawa na karibu Milioni 10 za Kitanzania, lakini mchumba wake Mary alimshawishi watafute fedha zaidi ili wafunge ndoa ya kifahari, ambayo pamoja na mambo mengine maharusi na wazazi wa pande zote mbili wangeletwa ukumbini kwa Helcopter za kukodi.

Mary alimuongezea Keneth Ksh 1 milion, sawa na milioni 20 za kitanzania, michango ya marafiki na jamaa ilifikia Ksh 2milion sawa na Milioni 40 za kitanzania na kiasi kilichobakia walikopa bank na kwa marafiki zao.

Inaelezwa kuwa walitarajia kulipa sehemu ya madeni hayo kutokana na zawadi za harusi ambazo wangepata, lakini hawakupata zawadi kubwa za kuweza kufidia madeni wanayodaiwa. Pamoja na kujiua, bank ya DTB imesema itapiga mnada nyumba ya wanandoa hao, iliyopo huko Nyalenda estate kufidia deni walilokopa bank.

Millar Ayo
 
Kila siku nawaambia vijana mwanaume hana haja ya kufanya sherehe ya harusi,, mwanaume anahitaji ndoa tu basi,,
Haya sasa kijana mwenzenu kashawishiwa kama Adam bustani ya Eden naye kaingia mkenge,,
Nawahurumia tu kwa kuwa wameamua kujitoa sadaka, hili game walitakiwa walicheze wakiwa hai ili iwe mfano kwa wengine,,
 
Back
Top Bottom