Bwana na Bibi shamba: Ama kweli, mganga hajigangi

x - mas

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
931
Reaction score
612
Habari ndugu wana jamvi,

Nina jambo hapa ambalo nataka tupeane uzoefu kidogo.Nashindwa kuelewa utaalamu ambao mtu kaupata kwa gharama na muda mwingi aumnufaishi ipasavyo. Pamoja kwamba bwana au bibi kilimo na ufugaji anajua vizuri kilimo na namna ya kupata mazao mengi na bora lakini chakustajaabisha wanao pata mafanikio katika sekta hiyo na kuwa mfano wa kuigwa ni wale ambao hawana utalaamu huo wa kusomea pengine hata form iv awaijui.

Mwisho wa siku wao wanakuwa ndio maboss wa hao wataalam wa Kilimo, tatizo nini hasa, nilitegemea wao ndio wawe mfano wa kuigwa lakini inakuwa ndivyo sivyo. Sijafanya utafiti rasmi lakini ndivyo inavyoonekana katika jamii yetu wataalam wa klimo/mifugo walio wengi wanamaisha ya kawaida wakati kuna watu ni mamilionea katika fani hiyo ijapokuwa awajaisomea.
 
Kwanza kabisa umeshasema kuwa haujafanya Utafiti,Na ki kanuni,ni kwamba Kama haujafanya utafiti hauna haki ya kuongea;Mkuu kwanza naomba ku-declare interest kwamba mimi mwenyewe ni Agriculturist,Baada ya hapo sasa nikujibu kwanini hali ipo hivyo,Mkuu ni kwamba Wengi wetu tuliosomea Kilimo huwa tunapenda kufanya Makubwa ktk Fani Yetu mimi mwenyewe nikiwa mmoja wao Lakini Kikwazo kikubwa ni Mtaji,Kutokana na kukosa mtaji ninashindwa ku-establish Mradi wa Kilimo cha Kisasa km vile Green house Farming,Ninashindwa pia kununua eneo zuri kwaajili ya Kilimo cha Kisasa na endelevu,Kutokana na kukosa mtaji ninashindwa Kununua vitendea kazi Madhubuti km vile Trekta,Maksai(Oxen),Mashine za Umwagiliaji pamoja na kutengeneza Miundo mbinu bora ya Umwagiliaji,Ninashindwa pia kuajiri Watu maalumu watakao nisaidia ktk kazi hizo za kilimo,n.k.,Hivyo mkuu siyo kwamba hatupendi au hatuwezi la hasha!,Changamoto ni hiyo,Ukisema ukakope benki na kwenyewe Magumashi Riba kubwa,Labda tutajaribu kwenye hiyo Benki ya kilimo tuone km itakuwa na riba rafiki kwa kilimo,Ushauri wangu ni kuwa Serikali wakitupa Support kidogo tutafanya Wonders hadi mtashangaa,Mimi nina future plan ya kuanzisha Kilimo cha Umwagiliaji Kwa kutumia Solar Power,Hivi sasa changamoto ni Mtaji na Mazingira,Japo ninaendesha kilimo hicho lkn si kwa Teknolojia ya juu kutokana na vikwazo nilivyovitaja,Ipo siku nitafanya makubwa ili kuondoa kabisa huo Mtazamo hasi wa mtoa mada.
 

si kwania mbaya au majungu ila nikutaka kujua nini hasa kinapelekea hali hii kutokea na yote haya inatokana na kuwa moja ya wadau wa kilimo hivyo katika halakati zangu nikaona ebu nililete hili nililo liona kwa wengi wa wataalamu wa kilimo.
Lengo ni kujua nini kinasabisha hilo hatahivyo nashukuru kwa kwani umeweza kubainisha kuwa mtaji ndio source ya wataalam wengi wa kilimo kutokufanya mikubwa,ingawa mimi nashindwa kutoa asilimia nyingi kwa hilo kwani miongoni mwa walio fanikiwa wengine walianza chini wengine hata kwa jembe la mkono lakini wamefika mbali sana.mfano ni ile stori ya vijana wawili wa morogoro ambao walianza ufugaji wa kuku kwa mtaji mdogo lakini hivi sasa wanashamba kubwa la kuku pamoja na mafanikio makubwa ikiwemo kumiliki magari manne na mpango wa kuanzisha shamba kubwa zaidi.
 
elim aliyo(tuliyo)ipata inamjenga mtu kuwa mkulima haswa na mjasiliamali, shidakubwa ni mitaji, ukiangalia mtu aliye ajiliwa analazimika kutumia galama kubwa ili afanikishe kwan mda wake mwingi yuko kazin, pia ieleweke kuwa bila kuandaa pesa yote utakayo itumia ktk uzalishaji mradi utaferi ,kwa mwenye taaruma ya kilimo hapendi aibu ya kufeli,wazo hili ndo kisababishi. hapo utapoteza kilakitu, hivyo, mtaji ni changamoto kubwa,
 

Nipo pamoja na wewe mkuu!,Niombee kwa Mungu huko ndiko napenda nielekee Mwanzo mgumu kamanda wangu.
 

Pamoja mkuu!.
 
tatizo sio mtaji, ni memtality yetu ndo shida, let start small and grow out capital to what we desire
 
Swali zuri sana ulilouliza. Na mkuu Ngamba amesena nitakachokirudia hapa.

Watanzania wengi hatupati elimu ya kujitemea bali tunapata elimu tegemezi.

Mimi nilipokuwa sekondari (ni siku nyingi sana, na kwa uzuri wako kwenye avatar yako sitasema ni lini) nilisoma na wahindi. Ilikuwa tukimaliza shule jioni sisi wamatumbi tulikwenda kucheza (gololi, mpira, nk.) wakati wenzetu walikwenda soma masomo ya biashara (bookkeeping, accountancy, management, nk.). Tulipomaliza shule (form 4, form 6, college) sote tulifuata taaluma zetu lakini wenzetu walikuwa pia na fikra za biashara. Hivyo ilikuwa rahisi kwa wao kuchepuka na kuanzisha biashara kufuatia mikondo ya taaluma zao kuliko mimi.

Sisi waswahili tulikuwa na mentality kuwa "kama umekwenda shule ina maana umeachana na jembe".

Hii iko katika fani zote. Ana degree ya:

Horticulture lakini hana hata bustani ya nyanya.
Veterinary medicine lakini hana hata veterinary clinic.
Mechanical Engineering lakini hana hata gereji ya kutengeneza magri.
Civil Engineering lakini hajui hata kupanga tofali kwenye banda la uani.
nk.

Fani zote hizi nilizotaja zinaweza kuanzisha biashara kubwa sana lakini hawana business skills za kuvulia nguo haya maji ya hizi biashara.

Sana sana wanaofanya vizuri siku hizi ni Lawyers na Madaktari-watu.

Oni langu ni kuwa mitaala yote ya elimu za ngazi za juu lazima ifundishe entrepreneurship/business skills. Watu wanaogopa hata kwenda benki kukopa hela za kuanzisha kabiashara kwa sababu hawajui kuwa wanaweza. Vijana wa darasa la saba walioelimishwa kuhusu biashara wanaju hiki kitu na wanafanikiwa.

Swali zuri sana uliloleta na ni changamoto kwa wizara yetu ya elimu. - Asante.

 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…