Bwana ni jumapili mpya ya tarehe 1/12/2024 asante Bwana kwa neema ya kuuona mwezi mpya

Magical power

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2022
Posts
2,158
Reaction score
5,626
Bwana ni jumapili mpya ya tarehe 1/12/2024 asante Bwana kwa neema ya kuuona mwezi mpya.
Bwana naomba mwezi huu ukawe ni mwezi uliobeba baraka na mashangilio tele ukawe mwezi wa kurejeshewa, kupata, kuinuka

Bwana hakika sisi na wanadamu ndani mwetu hatuishiwa mahitaji Bwana. Tunazo ndoto za maisha tuyatamaniyo kuyaishi Eee Bwana, tutendee wema wako na tunaomba utufanyie wepesi nasi katika kwikwi za matamanio yetu

Hakika wewe Bwana ni mwema kila wakati, ukuu wako hauchunguziki wala hauna mfano

Asante Bwana kwa zawadi ya maisha maana hii ndio zawadi kuu. Kuiona siku mpya ni neema zako tu, si ujanja wetu umetustahilisha

Bwana onekana katika kila eneo la uhitaji wetu, tutendee wema wako katika maisha yetu tunakuomba Eee Bwana ututende kwa ajili yetu .
 
Tumeomba na kushukuru, Amen🙏
 
Hakuna mungu, jipongeze maana umeona mwezi kwa juhudi zako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…