BWAWA LA UMEME JNHPP 1,075

BWAWA LA UMEME JNHPP 1,075

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
24,941
Reaction score
28,869
20 December 2024

BWAWA LA UMEME JNHPP Sasa linazalisha Megawatts 1,075 kati ya Megawatts 2115​



View: https://m.youtube.com/watch?v=uurfxrQkAi8

Vinu namba 9, 8, 7, 6 na 5 sasa vimekamilika hadi leo 18 December 2024 na huku vinu namba 4, 3, 2 na 1 kazi ya usimikaji inaendelea.

Kazi zote za usimikaji wa vinu vyote 9 na miundombinu ya usambazaji kuingia katika gridi ya taifa jumla ya megawatts 2,115 zitaingizwa katika gridi ya taifa .

Historia :
Mwaka 2021:
Dr. Medard Kalemani waziri wa Nishati : Ujenzi wa mradi huo JNHPP Stiegler's Gorge Rufiji umepangwa kukamilika Juni 14, 2022.

Mwaka 2022
January Makamba waziri wa NISHATI: Sisi tumeamua kusema ukweli bwawa la JNHPP litakamilika 2024

Mwaka 2024:
Dr. Doto Biteko waziri wa Nishati mwezi February 2024 amesema “Matarajio ni mradi huu kukamilika Desemba 2024 kwa mitambo yote tisa yenye uwezo wa kuzalisha Megawati 235 kila moja kuwa.

MRADI WA JNHPP UTAKAMILIKA MWEZI DISEMBA 2024 -NAIBU WAZIRI MKUU DKT.BITEKO​

Serikali imesema imeanza uzalishaji wa umeme kupitia mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia maji wa Julius Nyerere (JNHPP) wenye uwezo wa kuzalisha Megawati 2,115, ambapo uzalishaji huo umeanza kwa Megawati 235 kupitia mtambo namba tisa.

Hayo yamesema na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko Bungeni jijini Dodoma wakati akisoma hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Nishati kwa mwaka wa fedha 2024/2025.

“Matarajio ni mradi huu kukamilika Desemba 2024 kwa mitambo yote nane yenye uwezo wa kuzalisha Megawati 235 kila moja kuwa inazalisha umeme”. amesema Dkt.Biteko
 
Kazi nzuri.
Baada ya hili kukamilika waangalie vyanzo vingine vya umeme.
Upepo, jua, gesi nk
 
Kama mitambo 5 kati ya 9 imeshawashwa tayari na hali ya umeme ndo hii, basi ikiwashwa yote ndo tunaingia kwenye mgao mkuu!

Matatizo ya umeme kwa sasa;
  • Outage/Availability
  • Quality

Matatizo ya umeme miaka 30 iliyopita;
- Availability

Ndo kusema, mipango yetu haiendani na uhalisia wa ukuaji wa kimahitaji, hivyo badala ya kutatua matatizo, tunazalisha mengine mengi zaidi.

Kuna uwezekano wa kuwa kadiri Bwawa linavyoongeza uzalishaji, ndivyo vyanzo vilivyokuwepo awali vinakufa? Hivyo kuturudisha pale pale tunapotaka kutoka?

Story za umeme wa TZ ni uzalishaji na fedha, husikii wakizungumzia uboreshwaji wa usambazaji, miaka zaidi ya 60, unapambana kusafirisha umeme kwa vinguzo vya miti kwa umbali wa zaidi ya km 200, kweli?
- Gridi yenyewe ipo mikoa kadhaa tu.

Unaenda kutumia bilioni 30 kutengeneza APP ya kununua umeme, sijui token kufanya nini!
- Bilioni 30 zingeweza kuongeza 15MW ambazo zingelisha mkoa mmojawapo hapa Tanganyika.

  • Umekopa zaidi ya trilioni 39 kwa miaka 3, hakuna kitu tangible chenye kutatua shida za kweli za raia kimefanyika kwa pesa hizo, yet tuko serious na KUUPIGA MWINGI, mpaka 2030, blah blah blah....
  • Matokeo yake, wasomi wa jalalani wamekuwa chawa, msomi gani mwingine atapona kuwa chawa?
 
Back
Top Bottom