BWEGE MTOSENI

BWEGE MTOSENI

koncho77

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2014
Posts
7,789
Reaction score
10,388
RAFIKI: Vipi mbona leo huna
uchangamfu.

JAMAA: Wanawake bwana,
mwanamke hata umpendeje
atakugeuka tu.

RAFIKI: Nini tena ndugu yangu? Mbona shemeji mtu
fresh sana.

JAMAA: Hata mimi nilikuwa
najua hivyo, leo nimegundua
kumbe ana siri kubwa sana
ananificha, mimi naita huu ni usaliti wa ndoa.

RAFIKI: Nini tena?

JAMAA:Nimegundua mke
wangu kumbe anafanya
biashara ya kitimoto na
hajawahi hata kuniambia.

RAFIKI: Kitimoto? We
umejuaje?

JAMAA: Leo asubuhi
nilichelewa kuamka niliamua
nijipumzishe kidogo kabla ya
kwenda kazini, simu ya mke
wangu ikalia, nikaamua
kuipokea, kabla hata sijafungua mdomo, nikasikia sauti ya
mwanaume mmoja akauliza,

“Huyo nguruwe
umeshamuondoa?’ Hebu wewe
fikiria nilivyoshtuka, yaani
mpaka sasa nashindwa kuamini kuwa mke wangu ananizunguka
anafanya biashara ya nguruwe
hajaniambia hata siku moja.
 
Tangu lasaba wamalize mitihani na kuanza likizo ya kusubiri matokeo majumbani kwao JF sipaelewi elewi...kumekuwa na nyuzi za ajabu ajabu hivi..
Thank God matokeo yashatoka,wakienda shule kuanza form 1 zao nahs soon tutaendelea na JF yetu yenye viwango.....
Good luck kwa mkeo
 
Back
Top Bottom