Bweni la shule ya upili ya wavulana ya Migori lilishika moto jana usiku ambapo bidhaa za wanafunzi zilichomeka. Moto huo ulizuka wakati wanafunzi walikuwa kwenye masomo ya jioni. Ilichukua muda wa saa moja kuzima moto huo. Hakuna aliyejeruhiwa kwenye kisa hicho. Chanzo cha moto huo hakijabainika huku naibu mwalimu mkuu wa shule hiyo, Philip Rabongo akiwahimiza wazazi wawe watulivu kwani wanafunzi wote wako salama.