Yona F. Maro
R I P
- Nov 2, 2006
- 4,201
- 236
Ule utamaduni wa watanzania kutovumiliana na kuvunja sheria unaendelea tena usiku huu ambako wanafunzi wa shule ya sekondari ya Lugoba wilayani chalinze mkoa wa pwani wamefanya fujo na kuchoma bweni moja , mpaka sasa hivi haieleweki ni nini haswa chanzo cha fujo hizo mpaka kufikia kuchoma bweni hilo La wasichana moto pamoja na kufanya fujo zingine .
Pamoja na hayo kuna habari kwamba baadhi ya wasichana wamezimia kutokana na mshituko walioupata katika matukio yanayoendelea shuleni humo pamoja na fujo za hapa na pale .
Mpaka ninapoandika saa hizi walimu pamoja na baadhi ya wanafunzi wamefungiwa katika vyumba wengine wazimiwa simu zao za viganja pamoja na njia zingine za mawasiliano .
Hakuna polisi wala wanausalama wowote waliofika katika eneo la tukio mpaka sasa hivi wengi wa wanafunzi hao wamelala chini kungoja huduma ya kwanza .