Ibrah
JF-Expert Member
- Mar 22, 2007
- 2,730
- 530
Mlitutesa sana
Mlituumiza sana
Mlitutenga sana
Bye-bye DStv!
Mliringa sana
Mkaongeza matabaka
Ya walala hai
Na walala hoi
Bye-bye DStv
Bei yenu ilikuwa ghali
Kwa watu wa ghali
Mara dola sabini
Mara dola sitini
Bye-bye DStv
Leo nimekutana na tangazo la DStv katika kituo cha daladala hapa Arusha, sikuamini macho yangu. Ilibidi nisogee karibu na kuanza kulisoma kwa makini. NAdhani baadhi ya watu walinishangaa. Tangazo hilo lilinifanya nije na utenzi huo Byebye DStv!
Ati DStv sasa wamekuja na punguzo kwa wateja wao! Unapata channeli zisizopungua 25 kwa malipo ya shilingi 13,500/- kwa mwezi (vi9gezo na masharti yao kuzingatiwa!) Chaneli nyingi kati ya hizo 25 zinapatikana katika king'amuzi cha TBC; kuna TBN, TBC, Citizen, Trace, BeT nk. Chaneli za nyongeza ni ESPN, KBC, Gospel na Muslim.
Ilinikumbusha miaka ya ukiritimba na wizi waliotufanyia DStv kabla ya TBC kuja na ving'amuzi vya kichina-china. Walijipangia bei za ajabu-USD 60-70! Leo DStv wenyewe wamekubali yaishe. NAdhani watabaki wakiringia Super sports pekee ambayo ndo itawafanya wale wa madaraja ya juu kutupiga bao hapo lakini ikiwa TBC watalipia mechi zaidi za Premier League mwezi August ni wazi ngoma itakuwa droo.
Kwetu sisi wengineo ambao tuliwachukia DStv kwa ukiritimba na ubaguzi wao wa bei zao za kuruka, lau tumepata mahali pa nafuu kidogo.
NAkumbuka miaka ile ya kati ya 1990, DTV walikwa wakituonyesha mechi nyingi tu za Premier League kabla ya kuja hao DStv na kudai wao ndo wenye haki pekee ya kurusha mechi hizo Tanzania.
Hongera TBC,angalau kukomesha urasimu na majivuno ya DStv.