wajameni mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni!
hapa kuna mambo muhimu ya kuangalia mfano:
1) Mapinduzi yaliyoletwa na TBC/Startimes katika uangaliaje wa televisheni..zamani ilikuwa kwamba kuwa na DsTV ni kama ujiko flani na kama walivosema wengien ilikuwa inawakilisha watu wa 'class' fulani hivi...sasa hivi kuwa na king'amuzi cha startimes walau sio ajabu tena...walau kwa wale ambao wanafikiwa kwa sasa, DODOMA, DAR, MWANZA na Arusha.
2) Wenye DSTV sasa hivi, hata kama wanalipia 'chanel 25' lwa 13500 kwa mwezi bado ipo juu kulinganisha na startimes ambapo unapata channel zaidi ya 40 (mfano nina kama 48 hivi kwa sasa) kwa sh 9000 kwa mwezi. Kumbuka katika hizo channel pia zipo za filamu, michezo, muziki, watoto nk
3) Huhitaji watu wa startimes kuja kukufanyia installation manake hakuna dish..ni ka antenna kadogo tu mchezo umeisha. So kwa watu wa DSTV mauzo ya madish and the so called 'package' sasa hivi yatakuwa yanashuka
4)Tuendako, hata hizo channel za sports za super sports, zitakuwa zinaonyeshwa pia na TBC hivyo kuweka competition kubwa kabisa kwa watu wa DSTV. no wonder wameshusha bei gafla baad aya star times kuanza na huo ni mwanzo tu
5) Angalizo jingine ni kwamba TBC ni public owned sio state owned.