Cabinet Meeting......a month later and Karume Missing??


Point mzee. this one is good.
 

 
Kuna uwezekano mkubwa kuwa hiki kikao kilikuwa cha dharura kwa ajili tu ya kufahamishana kuhusu kupeleka majeshi Comoro otherwise labda kisingekuwapo(angalia article hapo chini).

Kama ni hivyo ina maana hakuna vikao vya mara kwa mara kupanga/kujadili/kufuatilia mikakati ya maendeleo inavyotekelezwa nk. Hii inatia wasiwasi uwezo na ubora wa uongozi wa Mh. JK. Hivi anaendeshaje nchi bila kukutana na timu yake? Hivi anaelewaje yanayoendelea kwenye wizara zake au kila waziri anafanya anavyoona yeye mwenyewe inafaa? Kazi kubwa tunayo, sura nzuri imetuponza.



 
[ Kama ni hivyo ina maana hakuna vikao vya mara kwa mara kupanga/kujadili/kufuatilia mikakati ya maendeleo inavyotekelezwa nk. Hii inatia wasiwasi uwezo na ubora wa uongozi wa Mh. JK. Hivi anaendeshaje nchi bila kukutana na timu yake? Hivi anaelewaje yanayoendelea kwenye wizara zake au kila waziri anafanya anavyoona yeye mwenyewe inafaa? Kazi kubwa tunayo, sura nzuri imetuponza.

Tungejuwa tungemchagua Mbowe awe Rais wetu
 

Not necessarily. CCM walikuwa na wagombea wazuri sana wawili kati ya finalist watatu. Lakini kwa mikwara iliyopo ndani ya CCM, akachaguliwa mbovu kati yao, kwa vile tu mwenyekiti, Mkapa, alitaka mtu wa kumlinda, mission town badala ya uchaguzi halali. Matokeo ndio haya tumeibua Vasco da Gama, wakati nchi ilikuwa inahitaji mchapa kazi mwenye kuona mbele.
 

MARAIS WALIOFUATIA ZANZIBAR BAADA YA IDRIS ...WAMEKUWA WAKOROFI KIDOGO KUHUSU KUAPA...LAKINI HISTORIA INAONESHA NA REKODI PALE IKULU ZIPO KUA BABA YAO ..YAANI..ABEID AMANI KARUME..ALIAPA KUWA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS ..NA MJUMBE WA BARAZA LA MAWAZIRI..MBELE YA MWALIMU..NA MARA ZOTE KARUME SR ALIONA FAHARI KUWA MAKAMU WA RAIS WA NCHI KUBWA TANZANIA.....

NADHANI TURUDISHE MAMLAKA YA RAIS WA ZANZIBAR KAMA MAKAMU WA RAIS ..WAZIRI MKUU ARUDI KUWA MAKAMU WA KWANZA AU WA PILI WA RAIS ....HII ITAMFANYA RAIS WA ZANZIBAR ASIWE INFERIOR ANAPOKUJA KWENYE BARAZA LA MAWAZIRI ...MAANA SASA SIMPLY ANAKUWA MSIKILIZAJI TU....NA KWA ZANZIBAR ILIVO NDOGO KUNA WAKATI RAIS WA ZANZIBAR SIMPLY ANAAMKA ANAKUWA HAJUI AFANYEJE..ZAIDI YA KUKAGUA MASHINA YA WAKEREKETWA KAMA ALIVYOKUWA SALMIN AU KUSHINDA NDANI ANAKUNYWA WHISKY NA KULALA KAMA AMANI.....

MTAGUNDUA KARUME SR NA ABOUD JUMBE NA HATA WAKIL..WALIKUWA WAKIZUNGUKA SANA MIKOANI TANZANIA YOTE ...NA KUWAKILISHA RAIS NJE ...KWA KUWA WALIKUWA NA KOFIA YA UMAKAMU WA RAIS....NAFIKIRI TURUDI KULE KAMA TUNATAKA MUUNGANO IMARA!!!
 
Kamanda taratibu hapo...!
 
Unajua topic zingine hata pa kuanzia huelewi, Karume anaweza kugoma kwenda kwenye mkutano wa serikali na CCM? Aliyempora urais Bilali na kumpa yeye ni nani? Hiyo jeuri Karume ataitoa wapi?

Ukweli ni kwamba sio lazima Karume, ahudhurie kila mkutano wa cabinet au CCM, Karume ni rais wa visiwani, kwa hivyo anazo schedule zake za kirais ambazo haziwezi kuvunjwa ki-protocal kwa sababu ya mikutano ya dharura ya CCM au cabinet, sidhani kama mtu anahitaji shule kuelewa hili!
 

Hii ni kumdhalilisha Karume kusema kuwa alipewa uraisi na sio kuwa ana-qualify. Muhimu ni kufahamu kuwa kama kikao kiliandaliwa siku kadhaa na sio cha kushtukizia, kwanini karume hayupo hasa ikitiliwa maanani kuwa raisi alitaka pia kuwaeleza kuwa vijana tayari wako Anjuan, Comoro?
 
Mkuu kuwepo au kutokuwepo kwa demokrasia ndani ya CCM, will never help any of your misery ambayo unaionyesha hapa kila siku na very angry comments, CCM ina katiba na mipangilio yake,

Halafu unaonekana kuwa mgeni sana na bongo, maana haya yalipotokea yalitangazwa kila kona ya bongo, sasa nina mashaka kama kweli wewe ni mbongo maana haiweezekani kila kitu huelewi, na huenda ikawa a waste of time hata kujadili ishus na wewe maana mengi sana huelewi yanayotokea bongo kila siku mkuu, nafikiri ninahitaji kuiangalia hilo kwa makini.

Ahsante Mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…