Shadida Salum
Journalist at JamiiForums
- Sep 11, 2020
- 69
- 105
Namungo FC watakutana uso kwa uso na Primeiro de Agosto ya Angola katika hatua ya mtoano ya mashindano ya Kombe la shirikisho barani Afrika.
Timu hiyo ya Ligi Kuu ya Tanzania ambayo inacheza mara ya kwanza katika hatua hii, itacheza ugenini kabla ya mechi ya nyumbani ambapo mchezo wa kwanza utachezwa Februari 12 na wa pili Februari 21.
Mshindi wa matokeo ya ujumla kwa Nyumbani na Ugenini atafuzu hatua ya Makundi ya mashindano hayo.
Namungo, chini ya kocha mpya Hemed Morocco ilipata nafasi katika hatua ya mchujo baada ya ushindi wa jumla ya 5-3 dhidi ya El-Hilal Obayed ya Sudan.
Stephen Kwame Sey, alifunga katika mchezo wa kwanza ambao walishinda 2-0, Blaise Bigirimana na Edward Charles Manyama walifunga mabao matatu muhimu kwa Namungo katika mchezo wa mkondo wa pili uliomalizika kwa sare ya 3-3.
Kwa upande mwingine, Primeiro de Agosto, aliangukia Kombe la Shirikisho baada ya kufungwa na Kaizer Chiefs 1-0 katika mchezo wa mkondo wa pili.