CAF Wakagua Miundombinu ya Michezo Kuelekea CHAN 2025

CAF Wakagua Miundombinu ya Michezo Kuelekea CHAN 2025

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
GZJgphgWAAA1ll9.jpg

Viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF) watembelea na kufanya ukaguzi katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Oktoba 5, 2024.

Viongozi hao wapo nchini kwa takriban siku mbili kuanzia Oktoba 5 kwa ajili ya kufanya ukaguzi wa viwanja mbalimbali vitakavyotumika kwenye mashindano ya CHAN 2025.

Aidha, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akiwa pamoja na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Gerson Msigwa aliwakaribisha viongozi hao huku akiwahidi ushirikiano wa kutosha kutoka Serikalini. @nsc_bmt@tanfootball

Maofisa hao wa CAF, wameriidhishwa na hatua iliyofikiwa ya Maandalizi na kupongeza juhudi za Serikali pamoja na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa utayari wao katika mashindano hayo, ambapo Tanzania, Kenya na Uganda ndio wenyeji.


GZJgphgWAAA1ll9.jpg
GZJgpgTXkAAbLH2.jpg
GZJgpgcXsAA_spT.jpg
GZJgpgUWsAA23_H.jpg
Screenshot 2024-10-06 at 18-13-07 Wizara ya Sanaa(MCAS) (@wizara_sanaatz) • Instagram photos a...png
 
Back
Top Bottom