CAF wamekiita kijeba cha Congo Brazzaville wakipime umri

MPUNGA

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2010
Posts
838
Reaction score
561
CAF wamekiita kijeba cha Congo Brazzaville wakipime umri
By: Shaffih Dauda / Posted: Saturday 5th November 2016



Shirikisho la soka barani Africa (Confederation of African Football) lipo mbioni kufanya uchunguzi kufatia madai ya Congo fanya udanganyifu kwa mumchezesha mchezaji anayedhaniwa kuvuka umri kwenye mechi za kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika kwa vijana wa U17.

Congo-Brazzaville imefanikiwa kufuzu fainali hizo zitakazofanya mwaka ujao huko Madagascar baada ya kuiondosha Tanzania raundi ya mwisho ya kuwania kufuzu.

Laikini Tanzania ilipeleka malalamiko yake ikidai wapinzani wao kutumia wachezaji waliovuka umri uliowekwa na Caf kwenye mashindano husuka.

Shirikisho la soka Tanzania (TFF) liliindikia Caf likitaka wachezaji wanaolalamikiwa kuvuka umri wafanyiwe vipimo vya kuhakiki umri wao.

Kwa upande wao Caf wamemtaja mchezaji mmoja Langa-Lesse Bercy kwa ajili ya kumfanyia vipimo kwasababu Namibia (litolewa na Congo) waliwahi kulalamikia umri wa mchezaji huyo.

Mkurugenzi wa tiba wa Caf Dr Boubakary Sidiki amethibitisha kwa kuiandikia barua TFF kwamba, Bercy ambaye alifunga magoli dhidi ya Namibia na Tanzania na kuisaidia nchi yake kufuzu, atafanyiwa vipimo November 18 jijini Cairo, Misri.

Bercy atasafiri hadi Misri aiambatana na daktari wake wakati TFF pia watatuma madaktari wao kwa ajili ya kushuhudia zoezi hilo la upimwaji wa mchezaji anayelalamikiwa.

TFF pia watalipia gharama zote zitakazohitajikana Caf.

Kwa mujibu wa kanuni za Caf, udanganyifu wa umri ni kosa ambalo linapelekea nchi husika kufungiwa miaka mitatu kushiriki mashindano ya umri husika.

Nchi nne zitakazofanikiwa kucheza nusu fainali ya mashindano hayo, zitakuwa zimefuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia chini ya miaka 17 zitakazofanyika India.
 
Ni jambo jema kwa soka letu na taifa kwa ujumla, kama ikithibitika mhusika kudanganya umri!
 
Ikithibitika jamaa ni kikongwe sisi (TZ) Tutafaidika vipi? au ishu ni kuwaharibia tu!
 
kwanini wasipimwe mwanzo wa mashindano?
 
Wampime na demu wangu ananiambia ana miaka 17 wakati sasa anasoma degree ya pili Mzumbe DSM. Inaniuma sana kwa kweli.
 
Heci ,mwambie na mdogowako huyo hapo home anavyodanganya vijana hapa mtaani,kwanza alisema yeye Bikra wakati washkaji washAtoboa,sasa kila mwaka besdei yake anasema ana miaka 18, yaani tangu 2009 mpaka leo anasema ana miaka 18?

Toa boriti hapo kwenu kwanza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…