CAF wamteua Ahmed Arajiga kuchezesha robo fainali ya Ligi ya Mabingwa (CAFCL) kati ya Pyramids FC na FC FAR

Hongera sana Ahmed Arajiga! Hakika unastahili pongezi kwa hii hatua uliyoifikia. Wewe kwa sasa ndiyo mwamuzi bora kati nchini. Na hili ni somo kubwa sana kwa wale mbumbumbu wanaokupuuza.
 
Game moja hivi sikumbuki ilikuwa ni AC Milan na team gani hakimu alikuwa ni huyu mwamba.
Sasa Gattuso alikuwa akitembeza boots sana kwenye zone yake.

Kuna kipindi Gattuso naye akakwatuliwa,akalalama huku akimtizama refa,jamaa akamuonesha ishara kuwa asimame aendelee na mchezo,wakati huo huyu refa alikuwa akikimbia kuelekea uelekeo wa mpira,acha Gattuso ainuke na kuanza kumkimbiza huyu refa,refa hana habari kuwa anakimbizwa bali na yeye anakimbia kufuatilia matukio ya mchezo.

Mwishowe ilimbidi Gattuso aendelee na mchezo maana jamaa bado njiani aliendelea kuwapungia wapuuzi wengine kwa ishara kuwaonesha wainuke waendelee na mchezo.

Hili tukio lilinifurahisha sana ukizingatia uvaaji wa Gattuso basi bukta ilionekana kuubwa na tizama yake km asikari wa Kiyahudi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…