CAF yaipa TAanzania uenyeji wa fainali za U17

CAF yaipa TAanzania uenyeji wa fainali za U17

Mapengo 17

R I P
Joined
Mar 28, 2014
Posts
1,229
Reaction score
610
Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika -CAF leo hii limeipa Tanzania uenyeji wa fainali za michuano ya Afrika ya vijana umri chini ya miaka 17 mwaka 2019.

Uenyeji huu ni hatua muhimu sana kwa Tanzania katika kukuza soka la vijana na kwa hatua hii Tanzania itacheza moja kwa moja fainali hizi.

Katika kuandaa kikosi bora cha kushiriki fainali hizi Tanzania, mwezi Juni mwaka huu TFF itaandaa mashindano ya Taifa ya vijana umri chini ya miaka 13 na wachezaji bora wa mashindano haya wataunda kikosi cha mwanzo cha Taifa kuelekea fainali za mwaka 2019.

TFF inamshukuru sana Rais Jakaya Kikwete na Mh. Fennela Mukangara Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa kufanikisha maamuzi haya, na inaamini ushirikiano huu wa Serikali na wadau wengine utafanikisha mashindano haya mwaka 2019.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Best Regards,
Baraka Kizuguto
MEDIA & COMMUNICATION OFFICER
Tanzania Football Federation - TFF
 
Yaani Tz, huwa haiishi maajabu eeee!! Hao vijana wa miaka 17, wako wapi, na hata hiyo program ya kuwaandaa iko wapi, Kipindi kile wanataka kupiga pesa za Brazil walisema kuwa ziara ile itatuletea mafanikio, yako wapi? Mpira sio operation tokomeza MABUSHA, unaamka leo na kusema kesho tunaanzia Bagamoyo kutoa tiba ya mabusha na matende, na ukafanikiwa, mpira ni uwekezaji wa muda mrefu, Wanazani kwa kufanyika hapa Tz, ndio itakuza soka?!! kwenye soka hakuna ujanja ujanja jamani!! wale watoto wa mtaani waliofanya vizuri wako wapi? Hata makocha hao wageni wanakula pesa wanajua kabisa hamna soka hapa, mtu miaka 20,ndio anaanza kufundishwa basic skills za mpira, wakati watu wanaanza hiyo kwenye age ya miaka 9!!!jitu limekomaa misuli huko hata flexibility kakuna, Tatizo la malinzi naye amekuwa mtu wa siasa nyingi vitendo hakuna!! kwa mpira huu hata kwa AFGANISTAN hatutoki!!!!!
 
Back
Top Bottom