Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,267
Shirikisho la soka barani Afrika CAF limemtaja mshambuliaji wa Simba SC Meddie Kagere, pamoja na mshambuliaji Emmanuel Okwi, ambaye msimu uliopita alikuwa sehemu ya kikosi cha Simba SC na kupata mafanikio kwa klabu kufika hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini kwa sasa anacheza Itthad Alex SC ya nchini Misri, kuwa miongoni mwa wachezaji 20 wanaowania tuzo ya mwanasoka bora Afrika kwa wanaochezea ligi za ndani kwa mwaka 2019. (African Interclubs Player of the Year)
Tuzo hizo ambazo hufanyika kila mwaka likihusisha jopo la wanahabari na wataalamu wa masuala ya soka chini ya shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika (CAF), zinatarajiwa kufanyika January 7, mwaka 2020 Citadel Azure, Hurghada nchini Misri.