CAF yamtema refa aliyekataa goli la Aziz Ki

Labani og

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2020
Posts
19,637
Reaction score
29,473
Shirikisho la soka Afrika (CAF) limefanya mabadiliko ya timu ya waamuzi kwenye mchezo wa kombe la Shirikisho kati ya USM Algers dhidi ya RS Berkane ambapo Mwamuzi wa Mauritania, Beida Dahane ameondolewa kwenye nafasi hiyo huku nafasi yake ikichukuliwa na Aziz Bouh Abdel naye wa Mauritania.

Dahane atakumbukwa kwa maamuzi yake ya utata kwenye mchezo wa robo fainali ya CAFCL kati ya Mamelodi Sundowns dhidi ya Young Africans Sc ambapo alikataa bao halali la kiungo wa Yanga Stephanie Aziz Ki na kuzuia sintofahamu na mashabiki wa soka barani Afrika.

Aziz Bouh Abdel ndiye Mwamuzi aliyechezesha mechi ya hatua ya makundi kati ya Yanga Sc dhidi ya Al Ahly mnamo Desemba 2, 2023 katika dimba la Benjamin Mkapa kwenye sare ya 1-1.
#KitengeSports

Nb: Yanga ni dude kubwa[emoji23]

 
katemwa hapo lkn fifa wamemchukua olympic wameona anafaa kwa matumizi..😃
 
Nb: Yanga ni dude kubwa
Dude kubwa la kulilia goli lililokataliwa. Dude kubwa la kushindwa kurudisha goli lililokataliwa, na ni Aziz ki huyo huyo aliyekuwa wa kwanza kukosa goli la penati na kuudhihirisha ulimwengu wa soka kwamba Uto ni dude kubwa la kulalamikia goli na ni dude kubwa la kufeli 😂😂
 
Mabadiliko ya kawaida mbereko fc wataifanya ni hoja ya kuamkia!
 
Yaaah mkuu...upo sahihi....yanga inatisha
 
Inawezekana jamaa kaomba apumzike akijiandaa kwenda Paris Olympics
 
Hizi tabia za kikekike za kujilizaliza zitaisha lini? Na hii inaonesha ni jinsi gani uto ni timu ndogo Afrika .

Timu kubwa haiwezi kukaa eda mwaka mzima kulilia goli lililokataliwa na refa.
 
huyo anastahili afungiwe kabisa tusimwone akichezesha hata mechi ya mchangani tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…