John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,374
Uongozi wa Klabu ya Simba umethibitisha kupokea taarifa kutoka Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kuwa inayotoa nafasi ya kuingiza mashabiki 35,000 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa wakati wa mchezo wa Kundi D, Kombe la Shirikisho dhidi ya RS Berkane ya Morocco.
Simba itakuwa mwenyeji wa mchezo huo, Jumapili Machi 13, 2022 ikiwa na deni la kulipa kisasi cha kufungwa mabao 2-0 katika mchezo uliochezwa mjini Berkane-Morocco, Februari 27.
Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba, Ahmed Ally amethibitisha taarifa za kuruhusiwa kwa mashabiki 35,000, idadi ambayo ni sawa na ile ya mchezo wa mzunguko wa kwanza dhidi ya ASEC Mimosas uliomalizika kwa mnyama kuchomoza na ushindi wa mabao 3-1.
“Tulitamani kupata ruhusa ya kuwa na mashabiki wengi zaidi uwanjani wakati wa mchezo wetu dhidi ya RS Berkane, lakini taarifa ya CAF imesisitiza lazima tuwe na mashabiki 35,000.
“Tuliwaombwa CAF kuwa na mashabiki 60,000, lakini wameturuhusu kuwa na idadi hiyo 35,000 ya mashabiki, hivyo tunawahimiza mashabiki wetu kufiwa Uwanjani ili kuzitendea haki nafasi hizo tulizozipata,” amesema Ahmed Ally.