Shadida Salum
Journalist at JamiiForums
- Sep 11, 2020
- 69
- 105
Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars ilikua na kibarua kizito cha kupindua matokeo dhidi ya timu ya Taifa ya Sudan baada ya kupoteza nyumbani bao 1-0 katika mchezo wa kwanza wa kufuzu fainali za CHAN uliochezwa tarehe 22 Septemba 2019.
Licha ya kupoteza nyumbani katika mchezo wa marudiano wa Oktoba 18, 2019 Stars iliipiga Sudan bao 2-1 na hivyo kutengeneza jumla ya bao 2-2 hali iliyoifanya Stars kufuzu fainali za michuano hiyo ya kwa faida ya bao mbili za ugenini.
Mashindano ya Championnat d Afrique des Nations (CHAN) yaliyo chini ya Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) yanahusisha wachezaji wanaocheza ligi za ndani za nchi zao.
Mashindano hayo yanajumuisha timu 16 zilizogawanywa kwenye makundi 4 , kundi A, B ,C na D ambapo kwa msimu huu Tanzania ipo kundi D na Zambia, Guinea na Namibia.
CAF imetangaza tarehe mpya ya mashindani hayo kuwa ni tarehe 16 Januari mpaka tarehe 7 Februari.
Awali machuano hiyo ilipangwa kuanza tarehe 4-25 Aprili 2020 lakini mnamo tarehe 17 Machi CAF ilisitisha michuano hiyo kufuatia mripuko wa COVID19.
Ethopia ilipata nafasi ya kuwa mwenyeji wa michuano hiyo kabla ya Shirikisho la Soka nchini humo (EFF) kuweka wazi kuwa hawakua tayari kuwa wenyeji wa mashindano hayo na baadaye Cameroon ilipewa nafasi ya kufanya hivyo.
Bingwa mtetezi wa michuano ya CHAN ni Morocco ambaye yupo kundi C na Rwanda, Uganda na Togo.