CAF yatupilia mbali rufaa ya Guinea dhidi ya Tanzania kufuzu AFCON 2025

CAF yatupilia mbali rufaa ya Guinea dhidi ya Tanzania kufuzu AFCON 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kupitia Kamati yake ya Nidhamu, limetupilia mbali rufaa iliyokatwa na Shirikisho la soka la Guinea (FGF) kufuatia kushindwa kwao na Tanzania katika siku ya mwisho ya mchujo ya kusaka tiketi ya kufuzu AFCON 2025.
IMG_2047.jpeg

Guinea iliangazia ukiukwaji wa taratibu za kiuchezaji kuhusu beki Mtanzania Muhamed Ibrahim Ame, ambaye inadaiwa alicheza na nambari ya jezi ambayo haijaorodheshwa kwenye karatasi rasmi ya mechi.

Pia, Soma: Tanzania hatarini kuondolewa AFCON 2025 baada ya kukiuka kanuni za Shirikisho la Soka la Afrika (CAF)

Shirikisho hilo pia linapanga kukata rufaa kwa mujibu wa kifungu cha 54 hadi 58 cha kanuni za nidhamu za CAF.
IMG_2044.jpeg

Katika mchezo huo wa mwisho, Tanzania iliichapa Guinea bao 1-0 mtanange ambao ulipigwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.
 
Back
Top Bottom