beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,880
- 6,368
CAG ameonesha mapungufu yafuatayo katika usimamizi wa mali za Mamlaka ya Serikali za Mitaa;
1. Kutokuwepo kwa Hati za Umiliki wa ardhi zenye thamani ya TZS. 1.14 trilioni katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa 27, kutokana na uzembe wa menejimenti za Halmashauri husika kutokupima ardhi zinazozimiliki. Hali hii inaweza kusababisha migogoro kati ya Halmashauri na wananchi kutokana na kuvamia maeneo hayo,
2. Magari 441 na pikipiki 228 zinazomilikiwa na Halmashauri 61 kutokukatiwa bima. Hali hii inaweza kuisababishia Serikali hasara pale inapotokea ajali
3. Magari 727, pikipiki 138 na mali mbalimbali 31 zinazomilikiwa na Halmashauri 113 zimetelekezwa kwa muda mrefu bila matengenezo hivyo kupunguza ufanisi wa kiutendaji na kuingizia Serikali hasara kwa kununua magari na pikipiki nyingine
4. Kutokuwekwa namba za utambulisho na kutohifadhiwa vyema kwa mali za kudumu zenye thamani ya TZS. 2.81 bilioni zilizonunuliwa na Mamlaka ya Serikali za Mitaa 18 hivyo kufanya mali hizo kutotambulika kirahisi na kuwa na hatari ya kupotea , na
5. Mali za kudumu, zikiwemo mashine za kufulia na fotokopi, tofali, nondo, vifaa vya hospitali na kompyuta zenye thamani ya TZS. 1.92 bilioni zilizonunuliwa na Mamlaka ya Serikali za Mitaa 10 hazitumiki.
Athari
Mapungufu haya yanaweza kupelekea upotevu wa mali za Halmashauri na kukosekana kwa thamani ya fedha katika ununuzi wa mali hizo. Pia, ukosefu wa hati za umiliki wa maeneo ya Halmashauri inachangia kuongeza migogoro ya ardhi katika Halmashauri husika.
Ushauri:
WAJIBU inashauri yafuatayo;
1. Halmashauri husika kufanya uhakiki wa mali zake zote na kuziingiza kwenye rejesta ya mali za kudumu na kuzitumia kikamilifu ili kuwepo na thamani ya fedha
2. Menejimenti za Halmashauri zihakikishe zinapima ardhi zinazomiliki kwa madhumuni ya kupata hati za umiliki kwa usalama wa ardhi hizo
3. OR – TAMISEMI iwachukulie hatua za kinidhamu wahusika waliosababisha uzembe wa kutopima maeneo yanayomilikiwa na Halmashauri, na
4. Halmashauri zihakikishe zinakatia bima magari, pikipiki, mitambo na mali nyingine zinazomiliki.
WAJIBU INSTITUTE