CAG: Kitambulisho cha NIDA kiwe kigezo cha lazima kwa Wanafunzi wanaoomba mikopo

CAG: Kitambulisho cha NIDA kiwe kigezo cha lazima kwa Wanafunzi wanaoomba mikopo

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere amependekeza Uongozi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu uweke mwongozo unaohitaji uwasilishaji wa NIDA kuwa ni lazima kwa Woambaji wote wa mikopo wenye umri wa zaidi ya miaka 18 na Waombaji walio chini ya umri wa miaka 18 wawasilishe watakapofikisha miaka 18 kwa ajili ya kulipwa awamu za mikopo zinazofuata lengo likiwa ni kuimarisha mfumo wa ukusanyaji madeni kwakuwa mfumo wa kutegemea namba za mitihani ya form IV inawafanya washindwe kukusanya madeni kwa Wanafunzi hususani waliojiajiri au kuendelea na masomo zaidi.

Kupitia Ripoti Kuu ya Mwaka ya Ukaguzi wa Mashirika ya Umma kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023, CAG amesema Bodi pia iwatake Wanafunzi wanaoendelea au wakopaji waliopo kutoa NIDA zao kabla ya kupokea mikopo zaidi na kuingia makubaliano na Wadau wa kimkakati ili kuimarisha ujumuishaji wa mfumo huo hii ni baada ya CAG kubaini Bodi ina deni la mikopo ya Wanafunzi lililoiva la Tsh. trilioni 2.10 hadi tarehe 30 Juni 2023 na imekusanya shilingi trilioni 1.29 (asilimia 62 ya mikopo yote iliyoiva) tangu mwaka 2006/07, hii ikimaanisha kuwa Tsh. trilioni 0.81 (asilimia 38) ya mikopo iliyoiva bado haijakusanywa.

“Ukosefu wa ushirikiano wa mifumo na Wadau wa kimkakati unachangia kushindwa kukusanya mikopo hii, hii inazuia HESLB kutoa mikopo kwa Wanafunzi wengine wenye uhitaji, ukaguzi wangu pia ulipitia utendaji wa urejeshaji mikopo, nilibaini kuwa Bodi haina utambulisho wa lazima na wa kutegemewa wa kipekee kwa Wanafunzi wanaopokea mikopo na kukosa mfumo shirikishi na Wadau wa kimkakati kama utaratibu wa kuwatafuta wanufaika”

“Kwa maoni yangu, kuongezeka kwa idadi ya Wanufaika wa mikopo kunahitaji zaidi kuwa na mfumo thabiti na wa jumla wa utambulisho kama Nambari ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA), utekelezaji wa NIDA kama hitaji la lazima utaiwezesha Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kuwafuatilia wakopaji ipasavyo na kuboresha ufanisi wa ukusanyaji wa mikopo, na hatimaye kuhakikisha uendelevu wa utoaji mikopo”.

PIA SOMA:
- Ripoti 21 za CAG zatua Bungeni kwaajili ya kuanza kujadiliwa
 
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere amependekeza Uongozi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu uweke mwongozo unaohitaji uwasilishaji wa NIDA kuwa ni lazima kwa Woambaji wote wa mikopo wenye umri wa zaidi ya miaka 18 na Waombaji walio chini ya umri wa miaka 18 wawasilishe watakapofikisha miaka 18 kwa ajili ya kulipwa awamu za mikopo zinazofuata lengo likiwa ni kuimarisha mfumo wa ukusanyaji madeni kwakuwa mfumo wa kutegemea namba za mitihani ya form IV inawafanya washindwe kukusanya madeni kwa Wanafunzi hususani waliojiajiri au kuendelea na masomo zaidi.

Kupitia Ripoti Kuu ya Mwaka ya Ukaguzi wa Mashirika ya Umma kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023, CAG amesema Bodi pia iwatake Wanafunzi wanaoendelea au wakopaji waliopo kutoa NIDA zao kabla ya kupokea mikopo zaidi na kuingia makubaliano na Wadau wa kimkakati ili kuimarisha ujumuishaji wa mfumo huo hii ni baada ya CAG kubaini Bodi ina deni la mikopo ya Wanafunzi lililoiva la Tsh. trilioni 2.10 hadi tarehe 30 Juni 2023 na imekusanya shilingi trilioni 1.29 (asilimia 62 ya mikopo yote iliyoiva) tangu mwaka 2006/07, hii ikimaanisha kuwa Tsh. trilioni 0.81 (asilimia 38) ya mikopo iliyoiva bado haijakusanywa.

“Ukosefu wa ushirikiano wa mifumo na Wadau wa kimkakati unachangia kushindwa kukusanya mikopo hii, hii inazuia HESLB kutoa mikopo kwa Wanafunzi wengine wenye uhitaji, ukaguzi wangu pia ulipitia utendaji wa urejeshaji mikopo, nilibaini kuwa Bodi haina utambulisho wa lazima na wa kutegemewa wa kipekee kwa Wanafunzi wanaopokea mikopo na kukosa mfumo shirikishi na Wadau wa kimkakati kama utaratibu wa kuwatafuta wanufaika”

“Kwa maoni yangu, kuongezeka kwa idadi ya Wanufaika wa mikopo kunahitaji zaidi kuwa na mfumo thabiti na wa jumla wa utambulisho kama Nambari ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA), utekelezaji wa NIDA kama hitaji la lazima utaiwezesha Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kuwafuatilia wakopaji ipasavyo na kuboresha ufanisi wa ukusanyaji wa mikopo, na hatimaye kuhakikisha uendelevu wa utoaji mikopo”
 
Basi mamlaka inayotoa vitambulisho hivyo isiweke kigezo cha kutoa vitambulisho kwa wenye miaka 18+, kwasbb wanafunzi wengi hivi sasa wanamaliza kidato cha sita wakiwa na miaka 16 au 17.
 
Wakiamu hawawezi kufeli kabisa. Baada
Screenshot_20240415_173027_Gallery.png
ya miaka kadhaa na mimi nimejaa kingi
 
Mheshimiwa Rais, Tunakuomba Ingilia Kati Ufukuzaji Wa Watumishi Wa Umma Katika Taasisi ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa( NIDA).

Kwanza Kabisa, Mh Rais Tunakupongeza Kwa Kazi Nzuri Unayoendelea Kuifanya kwa Nchi yetu na Serikali Yetu. Hongera sana sana Mh Mwenyezi Mungu aendele Kukubariki .
Mh Rais itakuwa ni jambo jema na la busara ukiunda Tume Huru uchunguzi dhidi ya Uongozi Katika Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa iliyo Chini ya Mkurugenzi (Ismail Rumatila )na Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Fedha ( Dorothy Mbena).

Takribani Watumishi 42 Ndani ya Mamlaka Wamefukuzwa kwa Vipindi Tofauti Chini Ya Mkurugenzi huyo na Bado Anaendelea Kutoa Hati za Mashtaka kwa Watumishi Waliobakia ndani ya Mamlaka . Hii Inaonyesha Dhahiri Bado Kuna Kundi Kubwa la Watumishi Wataendelea Kufukuzwa Kazi.

Watumishi Wanahukumiwa Kwa Makosa Mbalimbali na Wapo pia ambao hawakutenda Makosa hayo kabisa. Licha ya Vithibitisho Kuonyesha Dhahiri Kuwa Makosa Hayo Hawakuyatenda Mfano Mzuri ni Mtumishi Aliyekuwa Wilaya ya Igunga na Mtumishi Wilaya ya Sikonge. Hii inaonyesha ni kiasi gani Uongozi wa Taasisi Wameshindwa Kutambua Uaminifu ,Uadilifu, na Ufanyaji wao wa kazi uliobora wa Wafanyakazi wao kwa Miaka Yote wakitumikia Taasisi. Vijana Wa Waaminifu Wanahitajika kwenye Vitengo mbalimbali kwenye Utumishi wa Umma ila Uongozi wa Taasisi hii umeshindwa Kubaini Sifa Njema Za Vijana Inasikitisha kuwa Uongozi wa Taasisi hii Umeshindwa Kutambua hilo na Kuwafukuza Kazi.

Maamuzi ya Hasira Yaliochukuliwa Dhidi ya Watumishi Hawa na Utaratibu wa Ufukuzwaji Hazifatwi.
Mtu Akifanya Kosa la Kwanza Hupewa Onyo Kwa Mdomo akirudia Hupewa onyo kwa Barua baadae Anasimamishwa Kupisha Uchunguzi na sio Kufukuzwa bila Hatua na Utaratibu wa Kiutumishi kufatwa Hii Huibua Mashaka na Wasiwasi Juu ya Watumishi Kufukuzwa Bila Utaratibu wala Haki. Ni Dhahiri Wapo Wengine wengi kati ya 42 Waliofukuzwa Kwa Uonevu. Uamuzi wa Aina Hii Umeibua Wasiwasi Kwa Watumishi Waliobakia ndani ya Taasisi.
Hii Imedhibitisha Dhahiri Kuwa Kuna Watu Wanafukuzwa Bila Makosa na Ni Wafanyakazi Waaminifu ,Waadilifu na Watendaji Bora Sana Kazini. Uchunguzi Unaweza Kufanyika Juu ya Watumishi waliofukuzwa Katika Ngazi za Wilaya ambapo Walikuwa Wakitumikia Taasisi na Kubaini Kama Je Makosa Walioshtakiwa Nayo Waliyafanya na Kuhusika .
Kuwafukuza Watumishi Waaminifu Imedhihirisha Kuwa Hata Ukiwa Muaminifu ,Muadilifu na Mchapakazi Ipo Siku Pasi na Shaka Mtumishi yoyote anaweza Kufukuzwa Kazi Kwa Makosa Yaliyosababishwa na Wengine Pasi kuangalia Mwenendo wake wa kazi ,Uadilifu wake Wala Uaminifu wake kwa Miaka yote kazini .

Hii Inaleta Hofu Kwa Wafanyakazi Waliobakia Sababu Kama Wafanyakazi Waadilifu Wanaweza Kufukuzwa Kazi kwa Namna Hii Bila Makosa hata wafanyakazi Waadilifu Waliobaki Kwenye Taasisi Wanawezwa Kufukuzwa pia . Hii Itachangia Ufanyaji Kazi Wa Wafanyakazi Hawa Waliobaki Kuwa Mdogo na Wakusuasua na kutoamini tena Katika Uongozi Wa Nchi na Viongozi Unaowachagua Katika Taasisi hizi .

Mh Rais wewe ni Mama Kiongozi mwenye Huruma na Haki. Nina Imani Kuwa Huwezi Kuona Watumishi Vijana Walio Waadilifu na Waaminifu Wenye Kufata Miongozo ya Kazi Wanafukuzwa Kazi Bila Haki . Tunatumaini Katika Uongozi wako Ulio wa Haki Kuwa Wafanyakazi Ambao Hawana Makosa Wanastahili Kurudi Kazini Kwakuwa Wanategemewa na Taifa na Serikali ya Tanzania na Wafanyakazi Watakao Bainika na Makosa Watafutiwe Adhabu Mbadala ya Aina Nyingine Si Kuondolewa Kwenye Utumishi wa Umma.

Mh Rais Licha ya Nafasi Ndogo walizonazo Kwenye Utumishi wa Umma Bado wana nafasi na Mchango Mkubwa Katika Serikali yao na Taifa lao. Kwa Udogo huu walionao na Bado wana Morali ya Kulitumikia Taifa, Serikali na Mh Rais wetu Mpendwa Mama Samia Suluhu Hassan . Wewe ni Mama na Kiongozi Taifa na kwako wanaleta Matatizo yao wakiwa na na Imani na Matumaini Makubwa hutawaacha Mtaani wakiongeza Idadi ya Watu Wasio na Ajira ihali ni Watumishi Waadilifu na Waaminifu na Bado Wana Nia Njema ya Kulitumikia Taifa na Serikali yao Ikiongozwa na Mh Rais Samia Suluhu Hassan
 
Back
Top Bottom