Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Taasisi ya Masuala ya Uwajibikaji wa Umma (WAJIBU) imekuwa ikiandaa ripoti za uwajibikaji zenye lengo la kuongeza uelewa wa Wananchi kuhusu mambo muhimu yaliyoibuliwa kwenye Ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
WAJIBU imeandaa ripoti nne (4) kutoka kwenye ripoti za CAG za Mwaka 2022/23 ambazo ni:
Uzinduzi huo unafanyika leo Jumanne, Julai 16, 2024 katika Hoteli ya Royal Village, Jijini Dodoma.
Utouh: Kilichotokea Kenya kinaonesha kunahitajika uwajibikaji katika fedha za Serikali
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya WAJIBU, Ludovick Utouh amesema maamuzi yanayofanyika katika Serikali yanatakiwa kuendana na aina ya kiazi kilichopo na kuwa Vijana wa sasa ni tofauti na ilivyokuwa kizazi cha Miaka 20 hadi 30 iliyopita.
Anasema “Mfano Tumeona majirani zetu Kenya, wale Vijana wadogo wanaojita Gen Z wameonesha na kueleza kwa vitendo kile wanachokitaka, walisema wao sio kama baba zao, kwa maana hawwezi kukubali kuona vitu vinaenda bila ridhaa ya Wananchi.”
Anaongeza “Hiyo inaonesha Serikali zinalazimika kuwajibika zaidi katika kuhakikisha mapato na matumizi ya Serikali yanadhibitiwa na kutumika vizuri zaidi.”
Utouh ambaye ni CAG Mstaafu amesema hayo wakati wa Uzinduzi wa Ripoti za Uwajibikaji zenye lengo la kuongeza uelewa wa Wananchi kuhusu mambo muhimu yaliyoibuliwa katika Ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Dodoma, leo Julai 16, 2024.
Ludovick Utouh: CAG anatakiwa kukutana na Maafisa Masuuli wajue wapi wanapokosea
Akizungumza katika uzinduzi wa Ripoti Nne za Taasisi ya WAJIBU zinazogusia Ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya WAJIBU, Ludovick Utouh amesema kujua upande gani unakosea kuna umuhimu wa CAG kukutana na Maafisa Masuuli ili kujadili kuhusu matumizi ya manunuzi ya fedha za umma.
Amesema “CAG na Maafisa Masuuli wakutane ili wazungumze wajue wapi wanapokosea na kama kuna tatizo usuluhishi upatikane kwa faida ya maendeleo ya Nchi kwa kuwa pande hizo mbili zinatakiwa kufanya kazi kwa ukaribu ili kukwepa makosa kujirudia Ripoti za CAG.”
Amesema uwepo wa CAG ni jicho la Watanzania katika rasilimali zao na kuwa mapendekezo anayoyatoa anayafanya kwa nia njema, ni vizuri yakaheshimiwa na kutekelezwa.
Moses Kimaro: Wananchi wanaichukulia Bajeti kama mali ya Serikali na haiwahusu
Meneja Programu za Utafiti na Miradi wa Taasisi ya WAJIBU, Moses Kimaro anasema “Licha ya Serikali kuwa na mikakati ya kuitangaza Bajeti lakini bado asilimia kubwa Wananchi wanaichukulia Bajeti ya Serikali kuwa sio yao na haiwahusu jambo ambalo halitakiwi kuwa hivyo.”
-
Ameongeza “Bajeti inahusu maisha ya kila mmoja wetu, kila unachokifanya wewe Mwananchi utambue kinahusiana na Bajeti ya Serikali, fikra hiyo inatakiwa kubadilika na hiyo inachangia kukoseka kwa Uwajibikaji kwa Viongozi.”
Ametoa ujumbe huo wakati wa Uzinduzi wa Ripoti za Uwajibikaji kuhusu mambo muhimu yaliyoibuliwa katika Ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), leo Julai 16, 2024.
MAMBO YENYE VIASHIRIA VYA RUSHWA, UBADHIRIFU NA UDANGANYIFU KWA MWAKA 2022/23
Uchambuzi wa ripoti za CAG za mwaka wa fedha 2022/23, umebaini miamala mbalimbali iliyofanyika kwenye serikali na taasisi zake ilikuwa na viashiria vya rushwa, ubadhirifu na udanganyifu. Miamala hiyo imebainika kwenye maeneo ya ukusanyaji wa mapato, usimamizi wa matumizi ya fedha za serikali na ununuzi wa umma katika Mamlaka za Serikali za Mitaa, Serikali Kuu na Mashirika ya Umma.
Uchambuzi unaonesha kupungua kwa viashiria vya rushwa, ubadhirifu na udanganyifu kila mwaka kwa miaka mitatu mfululizo. Mwaka 2020/21, miamala yenye viashiria vya rushwa, ubadhirifu na udanganyifu vilikuwa na thamani ya shilingi trilioni 4.59, mwaka 2021/22 shilingi trilioni 3.08 na mwaka 2022/23 shilingi trilioni 2.41 katika Mamlaka za Serikali za Mitaa, Serikali Kuu na Mashirika ya Umma.
Hii inaonesha kumekuwa na jitihada katika kufuata sheria na kanuni za ukusanyaji wa mapato na matumizi ya fedha za umma kwa baadhi ya watendaji wa serikali na taasisi zake. Hata hivyo, uchambuzi unaonesha kuongezeka kwa viashiria vya rushwa, ubadhirifu na udanganyifu kwenye Mamlaka ya Serikali za Mitaa kati ya mwaka 2021/22 shilingi bilioni 297.86 na 2022/23 shilingi bilioni 499.96.
Kielelezo Na.1.
Mwenendo wa viashiria vya Rushwa, Ubadhirifu na Udanganyifu kwa Miaka Mitatu 2020/21-2022/23 (Shilingi Bilioni)

- Ripoti ya uwajibikaji ya Viashiria vya Rushwa, Ubadhirifu na Udanganyifu katika Taasisi za Umma
- Ripoti ya Uwajibikaji ya Utoaji wa Huduma kwa Jamii
- Ripoti ya Uwajibikaji ya Mapato na Matumizi
- Ripoti ya Uwajibikaji ya Taasisi za Usimamizi za Umma