CAG Ripoti: Matumizi NHIF yanazidi michango ya Wanachama

CAG Ripoti: Matumizi NHIF yanazidi michango ya Wanachama

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere amesema ukaguzi umebaini kuwa matumizi kutoa huduma kwa wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya yamekuwa makubwa ikilinganishwa na michango yao.

Katika mwaka 2021/2022 mfuko umepata hasara ya Sh189.65 bilioni ikilinganishwa na Sh93.6 bilioni iliyokuwapo mwaka uliotangulia.

Ameyaeleza hayo wakati akiwasilisha ripoti yake ya ukaguzi ya mwaka 2021/2022 Dar es Salaam Ikulu leo Machi 29, 2022.

"Pia mfuko umekuwa na mtiririko hasi wa fedha katika shughuli zake za uendeshaji, mwenendo huu unaonyesha kuwa michango inaongezeka kwa asilimia 12.9 wakati matumizi yanaongezeka kwa asilimia 24.6 mara mbili," amesema Kichere.

Amesema makadirio ya uwezo wa mfuko kujiendesha kwa Juni 30, 2021 unaonyesha kuwa mapato ya mfuko yataendelea kuwa chini ya matumizi kwa siku zijazo na mfuko utatumia ziada iliyokusanywa jambo ambalo litasababisha ukwasi kuwa hasi ifikapo mwaka 2025.

"Napendekeza kufanyiwa kazi kwa mapendekezo ya ripoti ya wataalamu na kutekeleza yaliyohitajika ili kurekebisha nakisi kama vile kuimarisha usimamizi wa utoaji huduma za afya.

MWANANCHI
 
Yan matuminzi yasiyo walenga subscribers wa NHIF yamekuwa makubwa, kuliko subscribers wenyewe.

Okay hi ndio sababu ya bima ya lazima kupigwa chapuo, Ili kuokoa nhif isife.

Tanzania ni shamba la bibi.
 
Leo CAG amekabidhi report kwa Rais lakini sijafanikiwa kupata taarifa za NHIF. Hii taasisi imekua na madudu mengi sana kama CAG hajaigusa hii taasisi bhs kuna jambo kubwa sana tumefichwa nyuma ya pazia.

Moja ya taaisisi zilizofanya vibaya kuanzia huduma, ufisadi ni hii NHIF. Ndugu zangu kuna taarifa zozote kuhusu hii taasisi?
 
Uko pia hasara ndugu pesa nyingi zimelipwa kwenye huduma za kujifungua wanaume 😂
 
Chonde chonde Serikal shughulikieni Mfuko wa Bima ya Afya kwa haraka

Vinginevyo CCM tutapata wakati mgumu sana Uchaguzi mkuu 2025

Ikumbukwe akina mama wanautegemea sana mfuko wa Bima ya Afya na akina mama hawa ndio wapiga kura wanaotumaimiwa na Chama tawala

Ramadhan kareem!
 
Kuna hospitali dawa zina bei utadhani umebadilisha figo. kwann kila jambo jema la umma linahujumiwa? Nani ataokoa hali hii?
Bei zinapangwa na NHIF mzee, kama huwez baki nyumban utibiwe na vigagula
 
Ukifuatilia vizur ni matumizi yasiyo ya huduma..

NHIF inatoa mikopo ya facility, kusajili vituo visivyo na sifa, pamoja na matumizi yasiyo ya lazima, huo mfuko unaish vip.

Magari, Office, Vikao, uzinduzi, semina nk..

Mbona wenzao hawafanyi hivyo?..
Hata wakichaj 10M per beneficiaries bado loss itakuwa ni ile ile

Acha ufeli tu....
 
Back
Top Bottom