Haya ndio matokeo ya vurugu za watani wa jadi. Game ya watani wa jadi wa Cairo,Misri inaenda kupigwa ikishuhudiwa na shabiki 30 badala ya nyomi ya zaidi ya watu elfu 50.
Timu zimeruhusiwa kuingiza mashabiki 15 tu kila mmoja wengine wamearuhusiwa kutazama kwenye runinga.
Hili ni somo kwetu Simba na Yanga. Ziko kauli za kichochezi zinazoweza kuleta uvunjifu wa amani. Baadhi ya timu imekuwa ikidai na kuwaaminisha mashibiki kuwa inarogwa. Wengine eti wakidai serikali inaibeba timu fulani. Ni vyema mkapambana na hali yenu badala ya kutafuta wa kumwangushia zigo
Upande wa marefa pia muwe makini sio tu kwa Simba na Yanga,bali ni kwa kila timu